Chama cha Soka Mkoa wa Pwani COREFA, kesho kitaendelea na ziara yake wilayani Rufiji kwa ajili ya ufunguzi wa Kituo cha Nne cha michezo kwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka 10, 15, 17 hadi 20 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Meja Edward Gowele.

COREFA chini ya Mwenyekiti Robert Munisi inaendelea na ziara hiyo ya kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto na vijana mkoa wa Pwani ikiwa hadi sasa imeshazifikia Wilaya tatu ambazo ni Kibaha, Mkuranga na Kisarawe kufungua vituo hivyo na kwamba kesho mpango huo unaendelea Wilayani Rufiji katika Uwanja wa Mabatini kuanzia saa mbili kamili asubuhi.

COREFA inaendelea na mpango huo wa kuweka vituo vya michezo kwa kila Wilaya kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana ambapo mwitikio huo umekuwa chachu ya kuinua matumaini ya vijana wengi ili kuweza kutimiza ndoto zao katika nyanja mbalimbali za michezo ambapo mwitikio wake umekuwa mkubwa kwa kila eneo.

”Tunafarijika kuona kwamba wadau wengi wamichezo wanafurahishwa na hiki ambacho tunakifanya kuibua vipaji vya vijana wetu, tumeshazifikia Wilaya tatu sasa ni zamu ya watu wa Rufiji kufurahia fursa hii, hivyo siku ya kesho ni muhimu kwao wajitokeze katika uwanja wa Mabatini kujumuika pamoja kwa ajili ya tukio hili kubwa.

Hata hivyo ziara hii ni endelevu kwani mpango mkakati wa COREFA ni kuhakikisha kwamba inazifikia Wilaya zote saba za mkoa wa Pwani kwa lengo la kuwa na vituo hivyo ili vijana waweze kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo kucheza mpira ,kujifunza uamuzi wa michezo hususani katika kipengele cha kusimamia sheria za uwanjani.


Imetolewa leo Septemba 09


Na Christina Mwagala


Meneja wa Habari na Mawasiliano COREFA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...