Katika uboreshaji wa upatikanaji wa maji katika eneo la Tabata Kisukuru, Kinyerezi, Kifuru na Kibaga Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaanza kunjenga miundo mbinu itakayowezesha upatikanaji wa maji katika maeneo hayo kwa kuainisha mipango ya muda mfupi na ya muda mrefu itakayoenda kuboresha huduma ya Majisafi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea na kuzungumza na wananchi, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu amesema wamejipanga katika uboreshaji wa maji ili kuhakikisha kila mwananchi anapata maji kwa wakati na kuondokana na mgao wa maji.

Amesema DAWASA imeweza kupata pointi katika eneo la King’azi B kwa ajili ya kujenga Pampu ya kusukumia maji itakayojengwa kwa wiki mbili itakayowezesha upatikanaji wa maji katika maeneo ya Kifuru na Bonyokwa ili wananchi waweze kupata maji kwa uhakika.

“Serikali kupitia DAWASA imekuja na mipango ya muda mfupi ya kuboresha upatikanaji wa maji, ambapo kwanza ni kuweka vituo vya kusukuma maji maeneo ya Bonyokwa na eneo la Kingazi B vitakavyosaidia kusukuma maji na kupeleka kwenye maeneo yenye miinuko," amesema Kingu.   

Akizungumza na wananchi wa Kisukuru amesema changamoto iliyokuwepo katika eneo hilo ni kutokana na tatizo la ufungaji wa Transifoma hivyo baada ya TANESCO kumaliza zoezi hilo wataweza pampu ya kusukumia maji itakayosaidia kuleta maji kwa uhakika.

“Niwatoe hofu wananchi wa Kisukuru kuwa changamto zote ninazichukua na na sisi kama DAWASA tunakwenda kuzifanyia kazi hivyo ili upatikanaji wa maji katika eno hili iwe historia” Alisema Kingu

Naye Meneja wa Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kinyerezi amesema Burton Mwalupaso amesema wanataka kuweka pampu ya kusukumia maji ya kuongeza msukumo wa maji na kuyapeleka katika maeneo yote yanayohudumiwa na hili bomba ambayo ni Mtaa wa King’azi, Kifuru, Msingwa, Kibaga na Kanga.

Amesema kumalizika kwa ujenzi wa pampu ya kusukumia maji itapunguza mgao wa maji ambapo wananchi watapata maji kwa wakati kwani mkusumo wa maji utakuwa ni mzuri.

Naye Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Tabata Mhandisi Ole Philemoni amesema wananchi wa Kisukuru wanatafutiwa suluhu la kudumu hivyo wameanza kutimiza malengo ya muda mfupi ili kuweza kupunguza mgao wa maji katika eneo hilo.

Naye Joachimu Minja mwananchi wa Mtaa wa King’azi B ameishuku DAWASA kwa kuja na wazo la kufunga pampu ya kusukumia maji kwani itakuwa ni mwarobaini wa mgao wa maji unaoendelea katika maeneo yao kwani wananchi wa eneo hilo wanateseka na pia wanafunzi hawawezi kwenda shule kwa wakati kutokana na upatikanaji wa maji kuwa haba.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Kiula Kingu akizungumza na wananchi wa Kisukuru katika mkutano wa mtaa huo wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya miradi ya maji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji katika eneo hilo.
Mkoa wa Kihuduma DAWASA Tabata Mhandisi Ole Philemoni akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kisukuru wakati wa ziara ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu alipofikaka ajili ya kutatua changamoto za upaikanaji wa katika eneo hilo.
Baadhi wananchi wa Kisukuru wakiuliza maswali kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu alipofika kwenye mkutano wa wananchi walikuwa wanataka majibu kuhusu upatikanaji wa maji katika eneo hilo.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu alipokuwa anatoa fafanuzi baadhi ya maswali.
Mwenyekiti wa mtaa wa Msingwa kata ya Bonyokwa Hassan Ngimbi akimkaribisha Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu kwenye ziara yake ya kukagua upatikanaji wa maji pamoja na changamoto zilizopo katika maeneo yanayohudumiwa na DAWASA. Wa kwanza kushoto ni Meneja mawasiliano wa DAWASA, Everlasting Lyaro
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu akizungumza na Mwenyekiti wa mtaa wa Msingwa kata ya Bonyokwa, Hassan Ngimbi alipotembelea katika mtaa huo kwa ajili ya kufanya ziara katika maeneo yanayozungukwa na mtaa huo.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu akizungumza mara baada ya wataalamu wa DAWASA kupendekeza eneo litakalojengwa pampu ya kusukumia maji wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya DAWASA itakayoweza kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo hayo.
Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kinyerezi amesema Burton Mwalupaso akitoa ufafanuzi kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu  alipotembelea eneo lililopendekezwa kujengwa kwa pampu ya kusukumia maji katika eneo la King'azi B.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu(wa pili kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa mtaa wa King’azi B, Bakari Ngorome (wa kwanza kushoto) kuhusu namna wananchi wanavyopata changamoto ya maji katika mtaa huo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kinyerezi amesema Burton Mwalupaso.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...