MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) wilayani humo kufanya uchunguzi kuhusu mradi wa maji wa Sh.bilioni moja uliokuwa ukitekelezwa na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) katika vitongoji 7 vya Kata ya Vumari.

Ametoa maagizo hayo wakati alipokagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo,ukiwemo miradi ya maji, ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Mbono unaotekelezwa na mradi wa Boost utakaogharimu. Sh.milioni 181.

"Rais Dkt Samiha Suluhu Hassani amejitahidi kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ikiwemo hii ya maji ambapo ametoa Sh.bilioni moja kwa ajili ya ukamilishwaji katika vitongoji hivi saba...

" Kwenye usimamizi wa miradi hii kuna changamoto na wananchi wanashindwa kunufaika na miradi.TAKUKURU mfuatilie haraka iwezekanavyo kuchunguza ili tujue ni kitu gani kinachofanya wananchi hawa wa vitongoji vitano kati ya saba wasinufaike na miradi ya maji na ni kwanini hayawafikii wananchi hao."

Pia Mkuu wa wilaya Kaslida Mgeni ametoa shukrani za dhati kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kw kuendelea kuwapatia fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na kuhakikisha fedha zinazo tolewa na Serikali zitatumika vema kwa kutekeleza miradi inayokusudiwa

Kwa upande wake Meneja wa Maji Wilaya ya Same Abdallah Gendaheka amesema kukosekana kwa maji katika vitongoji vitano ni kutokana na bahadhi ya wananchi kuharibu miundombinu ya maji lakini nradi huo mkandarasi alimaliza muda mrefu, hivyo amewaasa wananchi kutunza vyanzo vya maji

Bahadhi ya wananchi wa Kata ya Vumali wilayani Same Asha Abdallah na Herman Mgonja wamesema changamoto kubwa wanayopata ni Maji hasa kwenye hiki kipindi cha kiangazi ambacho wanaradhimika kunywa Maji yasiyo safi na salama.

Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni akizungumza na wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Wilaya hiyo ikiwemo miradi ya maji
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...