Na Mwandishi Wetu

MLEZI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Makongo, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Grace Mwashala, ameendelea na ziara yake  ya kuwawezesha wanachama wa umoja huo kwa kuwapa msaada wa bidhaa mbalimbali  vitakavyowawezesha kuanzisha miradi.

Diwani huyo  amekabidhi vitenge 55 kwa UWT Kata ya Makongo, ambapo ameutaka uongozi wa umoja huo kiviuza   kwa wanachama na wanawake  ambapo fedha zitakazopatikana zisaidie  umoja huo kujikwamua kiuchumi.

Pia, ametoa msaada wa kadi 333 za UWT, ambazo zitatolewa kwa wanachama na fedha itakayo patikana itaingizwa katika mfuko wa umoja huo ngazi ya Kata ya Makongo.

Akizungumza leo na UWT Makongo amewahimiza wanawake  kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali na  kubuni  miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Nimewapa hivi  vitu  uzianeni  na fedha iingie katika akaunti.  Wanawake tumuunge mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya. Anatuletea fursa nyingi za kiuchumi," amesema.

Pia amewahimiza pia umoja huo katika kata hiyo kuingiza wanachama wapya na ndiyo maana ameona umuhimu wa kutoa kadi hizo 333.

Mbali na msaada huo, Diwani Grace ametoa edha ya kufungua akaunti kwaajili ya shughuli hiyo ya ujasiriamali katika kata hiyo  huku akisisitiza wanawake kuwa wamoja, kupendana, kushikamana na kuungishana katika  biashara zao za ujasiriamali.

Kwa upande wake Katibu wa UWT wa Kata ya Makongo Deodata Komba, amemshukuru  diwani huyo kwa msaada huo na kuahidi kutekeleza maelekezo kwa kusimamia mradi huo kikamilifu. 

Tayari  Diwani Grace amekabidhi msaada kama huo katika Kata ya Bunju, jijini Dar es Salaam.

Mlezi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Makongo, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Grace Mwashala ( wa tatu kushoto) akimkabidhi  Katibu wa umoja huo  wa kata hiyo  Deodata Komba, msaada wa vitenge  55 na kadi za UWT 333 kwa lengo la kuanzisha mradi. Wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa UWT Kata ya Makongo Abriaty Kivea.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...