Na Janeth Raphael

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mhe. Deogratus Ndejembi amezitaka halmashauri nchini kuendelea kutenga Fedha Kwa kila mtoto chini ya miaka mitano Kwa asilimia 100 au zaidi Kwa ajili ya utekelezaji wa afua za lishe.

Mhe. Ndejembi amesema hayo leo Septemba 25, 2023 jijini Dodoma wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMASEMI. Mhe. Mohamed Mchengerwa kwenye Mkutano wa Tathmini ya Mradi wa Lishe Endelevu zoezi lililoenda sambamba na Uzinduzi wa Kitabu cha Kumbukumbu za Sauti za Walengwa wa Mradi wa USAID / Lishe  Endelevu na Kukabidhi Mradi Ngazi ya Taifa.

Mhe.Ndejembi amezitaka kusimamia kikamilifu utekelezaji wa masuala ya lishe kama yalivyobainishwa katika mpango jumuishi wa lishe wa mwaka 2021/22 mpaka 2025/26

"Halmashauri zihakikishe zinaendelea kutoa motisha Kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwani wao ndio nguzo kubwa ya utekelezaji wa afua za lishe,"amesema Ndejembi

Aidha amesema Tanzania imeweza kupiga hatua kubwa katika kudhibiti utapiamlo na ushirikishwaji wa wadau wa sekta zote ambao vipaumbele vyao vinachangia kuboresha hali ya Lishe na Afya ya Jamii nchini umekuwa ni nguzo ya mafanikio kwa nchi na uboroeshaji wa lishe ya jamii yetu ni suala mtambuka linalohitaji kila mtu, kila sekta na kila mdau ashiriki kikamilifu.

“Ninamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan kwa msukumo mkubwa aliouweka katika suala la kuwekeza katika lishe na hususan siku elfu moja za mwanzao za maisha ya mtoto ambapo siku 1000 zinapatikana kuanzia siku mimba inapotungwa hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili. Amesema Mhe. Ndejembi

Amesema Tanzania imepiga hatua katika kutokomeza udumavu matokeo ya utafiti wa Kitaifa(Tanzania National Demographic Health Survey -TDHS) WA MWAKA 2015/16 ilionesha udumavu ulikuwa 34% na mwaka 2022 udumavu umeshuka kufika 30%.

“ukiangalia Mkoa wa Dodoma na Rukwa ambapo Mradi wa Lishe Endelevu umetekelzwa kumekuwa na punguzo la udumavu kwa wastani wa 6% na 6.5.”ameeleza Mhe. Ndejembi

Hata hivyo Ndejembi amewataka viongozi wa serikali na chama kuhakikisha suala la lishe linatiliwa mkazo na kusimamiwa ipasavyo kama ambavyo imeelekezwa katika mkakati wa pili wa kitaifa wa kuboresha hali ya lishe (NMNAP II).

"Maafisa lishe, Maafisa kilimo na mifugo mmejengewa uwezo na mmepewa vitendea kazi,wasaidieni wananchi kutumia mbinu bora za kilimo na ufugaji lakini pia hakikisheni wananchi wetu wanatumia mazao hayo kula Ili kuboresha Afya na lishe ya familia zao,".

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulika Afya Dkt. Charles Mahera amesema suala la lishe watanzania wanatakiwa kulipa kipaumbele sababu lishe bora husababisha kuwa na afya bora na wananchi bora katika masuala mbalimbali kwa sababu lishe inasaidia ukuaji wa akili.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save The Children Tanzania,Bi.Angela Kauleni amesema Takwimu za hivi karibuni za tathimini ya hali ya Afya na makazi (TDHS 2020) zinaonesha kuwa watoto 30 kati ya 100 waliochini ya miaka mitano wanakabiliwa na udumavu ambapo hali hiyo huathiri ukuaji na kupevuka kiakili,kimwili na kisaikolojia Kwa watoto.

Aidha amesema kuwa  wataendelea kushirikiana na serikali kutekeleza malengo na mipango ya kimikakati ya maendeleo na hasa inayolenga Kuzuia udumavu na vifo vya watoto Chini ya miaka mitano, upatikanaji wa elimu bora Kwa watoto wote, ulinzi wa watoto na ustawi wa haki za watoto.

"Ili kufanikisha malengo haya Save The Children itazingatia vipaumbele vifuatavyo- kukuza sauti na ushiriki wa watoto na jamii katika masuala yanayowahusu, kuimarisha uhusiano wa kimkakati na wadau mbalimbali kuwekeza kwenye mipango na tafiti zinawezesha jamii na taifa kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi,"amesema Bi.Angela

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Raisi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Deogratius Ndejembi,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tathmini ya Mradi wa Lishe Endelevu zoezi lililoenda sambamba na Uzinduzi wa Kitabu cha Kumbukumbu za Sauti za Walengwa wa Mradi wa USAID / Lishe  Endelevu na Kukabidhi Mradi Ngazi ya Taifa hafla iliyofanyika leo Septemba 25,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Raisi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Deogratius Ndejembi,akipata maelezo mbalimbali kwenye mabanda wakati wa Mkutano wa Tathmini ya Mradi wa Lishe Endelevu zoezi lililoenda sambamba na Uzinduzi wa Kitabu cha Kumbukumbu za Sauti za Walengwa wa Mradi wa USAID / Lishe  Endelevu na Kukabidhi Mradi Ngazi ya Taifa hafla iliyofanyika leo Septemba 25,2023 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulika Afya Dkt. Charles Mahera,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tathmini ya Mradi wa Lishe Endelevu zoezi lililoenda sambamba na Uzinduzi wa Kitabu cha Kumbukumbu za Sauti za Walengwa wa Mradi wa USAID / Lishe  Endelevu na Kukabidhi Mradi Ngazi ya Taifa hafla iliyofanyika leo Septemba 25,2023 jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...