Na Humphrey Shao,Michuzi TV

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inaendelea kuhakikisha huduma za kibiashara hususani utoaji wa leseni za biashara  zinawafikia wananchi kwa wakati na mahali walipo,

Hayo yamebainishwa leo Septemba 18, 2023 na Mkuu wa Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw.Nikasi Msemwa wakati wa zoezi la utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara wa Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Bw. Msemwa ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la DSM imedhamiria kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa ukaribu zaidi  kwani wameweza kuanzisha kanda saba za kutolea huduma hivyo baada ya hilo wameanza kutoa leseni kwa wafanyabiashara kwa kuwafuata katika maeneo yao ya biashara.
Sambamba na hilo Bw.

"Zoezi hili limedhamiria kuwafikia wafanya Wafanyabiashara zaidi ya elfu 15 kwa Kariakoo ambao mpaka sasa wafanyabiashara elfu nane bado hawajapata leseni hivyo mpango mkakati huu wa kuleta huduma karibu yao utasaidia kukamilisha zoezi hili ambapo kwa Kariakoo zoezi hili litaendelea kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo tutaelekea kanda za pembezoni ila ikumbukwe kuwa utoaji huu wa leseni umeambatana na elimu ya jinsi ya kujisajili kwenye mfumo na namna gani ya kutumia mashine zetu katika utoaji wa risiti hivyo nitoe wito kwa wafanyabiashata wote kutumia fursa hii kujipatia leseni ya biashara papo hapo bila kusubiri na kwa Wafanyabiashara wote wenye taarifa hizi wafike maeneo ya huduma ili wapate leseni  zao pamoja na elimu kwa ujumla.” Amesema Msemwa.

Akitoa wito kwa Wafanyabiashara wenzake Bw.Julius Joseph Lullenge ametoa shukrani zake kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wataalamu wake kwa kuona tija kuhusu swala la leseni na kuwasogezea huduma hiyo karibu huku akiwahimiza wafanyabiashara wenzake kufika eneo la utoaji huduma na kupata elimu ya namna ya kutumia mashine kwani yeye amefika mahali hapo na ameweza kuelekezwa namna ya kutoa risiti kwa kutumia mashine za EFD na kuweza kuelewa pia ametoa wito kwa wafanyabiashara wenzake kutumia fursa kwa kupata leseni papo hapo na kujifunza kwa ujumla.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam  kwa sasa imefanya ugatuaji wa Madaraka kwa kujigawa katika zone jambo ambalo limesaidia kupatikana kwa huduma za kijamii kwa urahisi.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...