MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Morogoro imemhukumu Awadhi Hamza Mohamed adhabu ya kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana hatia kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kilogranu 34.65.

Aidha mahakama imeamuru kiasi hicho cha bangi kuteketezwa.

Katika hukumu iliyotolewa Agosti 31 2023 na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama hiyo Livini  Lykinana imeeleza kuwa, adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa sheria na pia ili iwe fundisho kwa wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Upande wa Jamhuri katika shauri hilo uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Elias Masini ambapo jumla ya mashahidi watano (5) wa upande wa Jamhuri waitoa ushahidi ambao umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa alisafirisha dawa hizo huku upande wa utetezi, mtuhumiwa alijitetea mwenyewe.

Hata hivyo, mtuhumiwa baada ya kusomewa adhabu hiyo aliomba Mahakama impunguziwe adhabu akidai kuwa hilo ni kosa lake la kwanza kutenda pia anafamilia ambayo inamtegemea yeye na l anamatatizo ya uti wa mgongo.

Mtuhumiwa alikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Desemba  22, 2022 katika kijiji cha Chogoali Sokoni kata ya Iyongwe, wilaya ya Gairo mkoani Morogoro akiwa na Kilogramu 34.64 za dawa za kulevya aina ya Bangi alizokuwa ameficha na kudhihifadhi katika mifuko ya sandarusi.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...