Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Afya na UKIMWI imezitaka taasisi zinazodaiwa na Bohari ya Dawa(MSD) kulipa madeni hayo ambayo kwa ujumla yanafikia zaidi ya Sh.bilioni 20 na miongoni wanaodaiwa fedha ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na MOI.

Ushauri huo umetolewa leo Septemba 13, 2023 jijini Dar es Salaam na Kamati hiyo baada ya kufanya ziara ya kutembelea maghala ya MSD Mabibo na Keko ambapo pia wameelezwa kufurahishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na bohari hiyo kuhudumia wananchi katika kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa tiba kwa wastani wa zaidi ya asilimia 90.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Stanslaus Nyongo wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo ya Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Afya na Ukimwi amesema wamefurahishwa na mikakati ya bohari hiyo lakini ni vema wanaodaiwa wakalipa madeni ili MSD iendelee kutoa huduma zake.

"Tumepata taarifa mbalimbali za MSD namna ambavyo wamejipanga kutoa huduma zao kwa wananchi lakini kunachangamoto ya madeni ambayo wanadai kwa wateja wao, hivyo tunashauri madeni hayo yalipwe...

" Hata hivyo katika kujadili madeni ambayo MSD wanadai kwa wateja wao tumeelezwa yanachelewa kwasababu nao wanasubiria kulipwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya( NHIF).

"Katika ziara yetu tunatarajia kwenda Bima ya Afya hivyo tutazungumza nao ili waweze kulipa fedha ambazo wanadaiwa.Kwa hiyo hili ni jambo ambalo tutalizungumza na kupata muafaka " amesema Nyongo.

Kuhusu maombi ya MSD kuomba mtaji kwa Serikali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema serikali ipo katika hatua ya mwisho ya kuipatia mtaji MSD na Bunge litaendelea kupigania uwezeshaji huo ufikiwe kwa haraka lengo likiwa ni kuijengea uwezo taasisi hiyo kwa maslahi ya taifa.

Amefafanua hali hiyo ndio msingi wa matokeo ya maborehso ya huduma bora za afya hatua ambayo pia itakayochea bohari kujenga maghala yake na kupunguza mzigo wa gharama ya kukosi, kuagiza, kusambaza na kuzalisha dawa na vifaa tiba ipasavyo.

"Kamati imejiridhisha namna MSD ilivyojipanga kimkakati katika uzalishaji wa dawa na kuweza kukua kwa taasisi hiyo kulingana na mahitaji yaliyopo.Hivyo wakati hayo yakiendelea ni vema wanaodaiwa na Bohari hiyo kanda ya Mashariki wakalipa madeni."

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel ameelezea hatua kwa hatua juhudi zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuiwezesha bohari hiyo na sekta ya afya kwa ujumla na kuhusu deni ambalo MSD wanadai kwa Hospitali ya Muhimbili na MOI.

Akielezea madeni hayo amesema tayari maelekezo yalishatolewa kuwa ndani ya siku 60 tangu huduma kufanyika deni lilipwe, hivyo hayo ni maagizo huku akifafanua watazungumza na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili nao walipe fedha wanazodaiwa na hospitali hizo.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai, ameeleza kwamba kwa sasa bohari imefurika shehena za dawa na vifaa tiba ambavyo vinaendelea kupakuliwa ukiwa ni mzigo ulioagizwa hivi karibuni.

“Kamati imekuja wakati mzuri tumetoka katika uagizaji tupo katika kupokea mzigo mkubwa wa vifaa vya afya, sasa miradi yote iliyokuwa na changamoto hususani ya vifa tiba kuna shehena ya kutosha kontena zinaendelea kushusha mizigo na tumewaeleza tulipotoka tulipo na tunapokwenda.

“Hatuongelei mikakati tena tupo katika utekelezaji tumeboresha mikataba ya uagizaji bidhaa, upatikanaji na uhusiano wetu na washitiri kwa kugatua MSD, kuboresha uwajibikaji na miundombinu kwa kujenga maghala mapya ambapo Dar es Salaam tunalipa bilioni 2 kwa mwezi kukodi ghala moja hivyo ni lazima tujenge ya kwetu,”amesema

Aidha amesema kutokana na kupungua kwa mtaji wa bohari hiyo Serikali inaendelea na hatua za utekelezaji za kuipatia fedha ambapo Wizara ya Fedha ipo katika mchakato wa mwisho na matumaini yaliyopo ni makubwa lengo ni kuhakikisha huduma za afya nchini zinakidhi mahitaji yaliyopo.

Mavere amesema katika kuhakikisha bohari hiyo haiwi mzigo kwa serikali wanaendelea na mchakato wa kushirikisha sekta binafsi katika uzalishaji.

Awali Meneja wa MSD Kanda ya Mashariki Betia Kaema alisema kanda hiyo inayohudumia Mikoa ya Pwani na Zanzibar ina changamoto kubwa ya kukosa eneo la ghala linalokidhi viwango na madeni wanayowadai wateja wao.

“Kamati imetushauri kufuatilia kwa kina madeni yaliyopo kwa kuwa yanakua kwa kasi, hadi sasa kanda inadai zaidi ya sh. bilioni 20 na sisi ili tupate dawa na huduma ziendelee ni lazima tulipe supply...

"Tumepokea maelekezo na tutaendelea kuzungumza na tunaowadai waweze kutulipa na sisi tuweze kujiendesha,”ameseema Kaema na kusisitiza kwa sasa usambazaji dawa na vifaa tiba umeimarika na hivyo kupunguza malalamiko kama ilivyo huko nyuma.

Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam Betie Kaema akieleza jambo kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayohusika na Afya na UKIMWI kufanya ziara katika bohari za kanda hiyo
Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Afya na UKIMWI wakiangalia baadhi ya vifaa tiba katika ghala la kuhifadhi dawa katika Bohari ya Dawa( MSD) Mabibo jiiini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 13, 2023 jijini baada ya Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Afya na UKIMWI kufanya ziara Bohari ya Dawa( MSD) Kanda ya Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa MSD Mavere Tukai akifafanua jambo kwa waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge
Matukio mbalimbali katika picha baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge inayohusika na Afya na UKIMWI

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...