KAMISHNA  Jenerali  wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amekutana na kufanya mazungumzo na  Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk. Benson  Bana.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Septemba  25, 2023 Kamishna Jenerali Lyimo na Balozi Dk.Bana wamejadili kwa kina kuhusu namna bora ya kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya kati ya Tanzania na nchi za Afrika Magharibi. 

Balozi Dk. Bana, pia  anawakilisha nchi 14 zilizopo ukanda magharibi mwa Bara la Afrika.Nchi hizo ni  Mali, Togo, Ghana , Guinea-Bissau, Guinea,  Mauritania, Niger, Cote d' Ivoire, Burkina faso, Gambia, Senegal, Liberia, Bennin , na  Siera Leon, 

Kamishna Jenerali ambaye ameambata na ujumbe kutoka Tanzania,  nchini Nigeria kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Vyombo vinavyopambana na Dawa za Kulevya kwa Nchi za Afrika HONLEA AFRICA 31, ambao unafanyika kuanzia  Septemba 25 hadi 29 Septemba 2023 jijini Abuja. 

Tanzania iliwahi kuwa mwenyeji wa Mkutano HONOLEA AFRICA Septemba 28 mwaka 2018.



Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo(kulia) akimsikiliza kwa makini Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk.Benson Bana baada ya kukutana na kufanya mazungumzo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...