KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Mzee Ramadhani Nyamka (Vazi suti nyeusi) akiwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili - Taasisi ya Mifupa (MOI) leo Septemba 30, 2023 kuwajulia hali baadhi ya majeruhi wa ajali ya treni iliyogongana na Basi la Jeshi la Magereza jana jioni katika eneo la Sabasaba, Ukonga Jijini DSM. Katika Ajali hiyo askari wa Jeshi hilo Sajini wa Magereza Twalib Sultan alipoteza Maisha, baadhi ya askari walijeruhiwa na mfungwa Mmoja.
Pix 2. KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Mzee Ramadhani Nyamka (Vazi suti nyeusi) akimjulia hali Mfungwa wa kunyongwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili - Taasisi ya Mifupa (MOI) leo Septemba 30, 2023. Mfungwa huyo na baadhi ya majeruhi(Askari) walipata ajali ya treni iliyogongana na Basi la Jeshi la Magereza jana jioni katika eneo la Sabasaba, Ukonga Jijini DSM.
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Mzee Ramadhani Nyamka (Vazi suti nyeusi) akimjulia hali majeruhi wa Ajali ya treni(SSGT Sebastian Mjata) ambaye ni Dreva wa Basi la Jeshi la Magereza lililohusisha katika ajali ya treni iliyotokea jana jioni katika eneo la Sabasaba, Ukonga Jijini DSM. Askari huyo anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Amana jijini DSM.
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Mzee Ramadhani Nyamka (Vazi suti nyeusi) akimfariji mfiwa ambaye ni Baba yake mzazi na Marehemu SGT Twalib Sultan ambaye alifariki jana katika Ajali hiyo. CGP Nyamka amefika nyumbani kwa Marehemu Ukonga Jijini DSM kwa lengo ya kuwafariji wafiwa. Picha zote na Jeshi la Magereza.

KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Mzee Ramadhani Nyamka (Vazi suti nyeusi) leo Septemba 30,2023 ametembelea eneo la Ajali iliyohusisha Basi la Jeshi hilo ambalo liligongana na Gari Moshi jana jioni, Sabasaba, Ukonga Jijini DSM. Jenerali Nyamka amewataka Madreva wote wa Jeshi la Magereza kuhakikisha kuwa wanazingatia Sheria za Usalama Barabarani ili kuepusha ajali zisitokee.
MWENYEKITI wa Mtaa wa Sabasaba, Ndugu Khalid Kivinga(kushoto) akitoa ushuhuda namna Ajali ilivyotokea mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Mzee Ramadhani Nyamka (Vazi suti nyeusi) alipotembelea eneo la Ajali hiyo leo Septemba 30, 2023 jijini DSM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...