Na Shalua Mpanda, TMC 

JITOHADA za viongozi wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam katika kampeni za usafi zinazofanyika mara kwa mara zimewagusa wadau mbalimbali na hatimaye kuunga mkono kampeni hizo.

Akizungumza katika zoezi la usafi lililofanyika leo tarehe 30 Septemba, 2023, katika Kata ya Miburani eneo la Temeke mwisho, Mkuu wa Wilaya Temeke Mobhare Matinyi amesema karibu kata zote 23 za wilaya hiyo zimepata wageni rasmi kutoka kada na sehemu mbalimbali.

Matinyi ameongeza zaidi kuwa kwa kuvutiwa na usafi wa mazingira wilayani humo, kampuni ya fedha ya Bayport imetoa miche ya miti 500 iliyopandwa  Septemba 29,  2023 wilayani humo wakati wa kuhitimisha awamu ya kwanza ya usafi ya mitaro na mifereji.

Matinyi ameongeza "Wakati tunazindua wiki ya kusafisha mitaro na mifereji, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayesimamia Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jaffo, alikuja kutuunga mkono kwa sababu aliona tunafanya jambo jema na wana Temeke tuna mwamko."

Kabla ya hapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, alikuwa mgeni rasmi kwenye siku ya usafi duniani wilayani humo ambamo iliadhimishwa kwa kufanya usafi kwa wiki nzima huku akitoa wito kwa wengine kuiiga Temeke.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Miburani Ali Kiaka ametoa rai kwa wananchi wa maeneo hayo kuendelea kutunza mazingira na kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mitaro na mifereji.

Mkuu wa wilaya ya Temeke mheshimiwa Mobhare Matinyi(katikati mwenye fulana nyekundu)akishiriki zoezi maalum la usafi na wananchi wa kata ya Miburani Temeke(Picha na Matthew Jonas-TMC)









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...