Na Said Mwishehe, Michuzi TV

UJUMBE wa wawakilishi wa kibiashara takribani 100 ukiongozwa na Baraza la Mkoa la Zhejiang nchini China unatarajia kuwepo nchini kushiriki  kongamano la kufanya tathimini eneo la viwanda kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza leo Septemba 4,2023 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa SinoTan Industrial Park, Janson Huang amesema ujumbe huo utashiriki mkutano huo utakaonza Septemba 25 mwaka huu na unatarajiwa kuwa na washiriki 500 kutoka kampuni mbalimbali.

Amesema wawakilishi hao wanatoka China, Angola, Kenya, Ethiopia na Tanzania na kusisitiza katika uhamasishaji wa biashara ya kimataifa ujumbe wa Serikali ya Watu wa Jinhua utatembelea Tanzania na Septemba 25.

Huang amesema ujumbe huo utakaa na wenzao wa Tanzania kufanya tathimini eneo Viwanda la China na Tanzania chini ya mwongozo wa Ubalozi wa China nchini.

“Wakati wa mkutano huo pia watazungumza kuhusu uwekezaji kati ya nchi hizi mbili na tayari katika kampuni hizo 100 ziko ambazo zimeanza kuonesha nia ya kutaka kuwekeza Tanzania,”amesema Huang.

Pia mkutano huo utahusisha watu kutoka serikalini na watatumia nafasi hiyo kuangalia fursa zinapaswa kupewa kipaumbele katika uwekezaji.

Aidha amesema mwamko wa kampuni za China kuja kuwekeza Tanzania unatokana na uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambao umeendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) John Mnali amesema kongamano hilo litaongeza kasi ya uwekezaji.

 Amefafanua kuanzia mwaka 1997 hadi 2023 China imewekeza miradi 1,134 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 10.5 na imetoa ajira 136,204.

Awali Mwakilishi wa Ubalozi wa China Yang Zeyu amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi zote zinaonesha nia ya kuchangia ukuaji wa uchumi na huduma za kijamii.

Amesema mwaka 2024 nchi za China na Tanzania zinatimiza miaka 60 ya ushirikiano wa kidiplomasia hivyo kinachofanywa na kampuni kutoka Zhejiang-Jinhua ni kuendeleza ushirikiano uliopo.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Leodgar

Tenga amesema watatumia kongamano hilo kujifunza mambo mbalimbali ambayo China imepitia hadi kufika hapo walipo.

“China imepiga hatua katika sekta ya viwanda na wawekezaji wetu wa ndani  wanapaswa kujitokeza kwa wingi Septemba 25, ili wabadilishane ujuzi,”amesema Tenga.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka TPSF Kinanasy Seif amewaomba wadau kutoka sekta ya viwanda kujisajili na kushiriki kongamano hilo.

Mkurugenzi wa Umasishaji na Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania( TIC) John Mnali(wa tatu kushoto) akizumgumza n waandishi wa habari kuhusu Kongamano la Tathimini eneo la viwanda kati ya Tanzania na China litakalofanyika Septemba 25 mwaka huu na kuhusisha kampuni 500 na kati ya hizo kampuni 100 zinatoka China





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...