NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KAMPUNI ya Kimatifa ya Utandazaji wa Mabomba ya Maji (AFCONS) imeiomba Serikali iendelee kuiamini kampuni hiyo kwani imekuwa ikijiyahidi kutekeleza miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikiingia na Serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa maji nchini.

Akizungumza leo Septemba 25,2023 Jijini Dar es Salaam, katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Bodi na Menejimenti za Mamlaka za Maji Tanzania Bara, Meneja wa Usambazaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Utandazaji wa Mabomba ya Maji AFCONS Bw. Jishin Chandra V amesema tatizo la Maji limekuwa changomoto, hivyo kupitia AFCONS na kuendelea kuaminiwa wataendelea kufanya vizuri kwani wamekuwa wakifanya kazi katika nchi mbalimbali barani Afrika.

Amesema Kampuni hiyo ipo katika nchi ya Msumbiji, Zambia, Madagascar, Zimbabwe, Benin, Gabon, Mauritius Ivory Coast, Mauritania, Ghana, Rwanda, Liberia pamoja na Tanzania ambapo kote wamekuwa wakiingia mikataba na Serikali katika kuhakikisha wanatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo miundombinu ya Reli, Madaraja pamoja na miundombinu ya Maji ambapo wanatekeleza nchini Tanzania.

"Tatizo la maji kwenye nchi yetu ni kubwa Sana kwa sababu nchi yetu ni kubwa sana, changamoto kubwa Sana iko vijijini mfano pale chaalinze Changamoto ilikua kubwa Sana Ila Sasa wananchi wanafurahia maji na serikali yao". Amesema 

Amesema mpaka sasa wameshaingia makubaliano ya ushirikiano na Serikali katika kutekeleza miradi ya maji ikiwemo mradi wa Maji Chalinze, Nzega, Mradi wa Maji Zanzibar pamoja na miradi mingine ambayo tayari imeshakamilika.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...