Na. Mwandishi wetu – Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuyajali makundi maalum ya vijana, Watoto, wazee na wenye ulemavu.

Mhe. Patrobas Katambi amesema hayo Septemba 6, 2023 katika Mkutano wa Maafisa Ustawi wa Jamii uliofanyika Jijini Dodoma ambapo Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye amefungua Mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa hao kutoka Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na sekta binafsi zinazotoa huduma za ustawi wa jamii nchini..

Amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa makundi hayo aliunda Wizara mahsusi kwa ajili kushughulikia masuala yanayohusu makundi hayo ikiwemo Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu na Ofisi hiyo.

Aidha, amewasisitiza Maafisa Ustawi wa Jamii kutambua matatizo na changamoto zinazokabili makundi hayo na kuwa na uwezo wa kutatua changamoto hizo kwa kutumia rasilimali zilizopo.



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi Septemba 6, 2023 akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na sekta binafsi zinazotoa huduma za ustawi wa jamii nchini, wa pili kushoto ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kulia) Septemba 6, 2023 akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko alipo wasili katika Mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na sekta binafsi zinazotoa huduma za ustawi wa jamii nchini.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (wa tatu kulia) Septemba 6, 2023 akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko (wan ne kulia) katika Mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na sekta binafsi zinazotoa huduma za ustawi wa jamii nchini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...