*Aslay kusherehekea miaka 10 na nyimbo 100 Septemba 30 dar*
 
Na.Khadija Seif Michuziblog 

MIAKA 10 ya Msanii Aslay awahaidi mashabiki wa Muziki wa live kukata kiu yao athibitisha Mbosso kutohudhuria Tamasha lake  "Miaka 10 + wimbo 100 litakalofanyika ukumbi wa Warehouse Masaki Jijini Dar es Salaam. 
 
Akizungumza na Wanahabari Leo Septemba 25,2023  Jijini Dar es Salaam akitambulisha rasmi Tamasha  lake Aslay amesema ukimya wake katika kiwanja cha muziki ulikua una mengi jambo kubwa akiweke bayana kutokuwa na wasimamizi wake wazuri wa muziki wake.

"Wote tunajua nilikua kimya kwa muda mrefu mashabiki zangu wamekuwa wakijiuliza maswali pengine majibu yao wengi yamekuwa hayapatiwi uthumbuzi hivyo Tamasha langu la "Miaka 10 +Nyimbo 100 kutokana na Menejimenti yangu mpya ya Rockstar". 

Aidha Aslay amewataja wasanii watakaosindikiza Tamasha hilo 'The art band' kutoka Kenya, Nandy, 'Enock bella', Abby charms, Harmonize, Ommy Dimpoz huku akitolea ufafanuzi kwa baadhi ya wasanii kutohudhuria akimtaja Kiba na Rafiki yake wa karibu Mbosso khan kuwa hawataweza kuhudhuria Tamasha hilo kutokana sababu zilizo nje ya  uwezo wao.

"Sijachagua wasanii ambao niliwahi kufanya nao kazi tu hapana ila nimeweza kukaribisha wasanii wengi tuweze kufurahi pamoja katika safari yangu ya mafanikio lakini kutokana na shughuli mbalimbali zinazoendelea kwa sasa imekuwa ngumu kwa Mbosso kuweza kujumuika kutokana na sherehe za Wasafi festival alikadhalika kwa upande wake Alikiba imeshindikana kutokana na majukumu mengi lakini wote ni watu wangu wakaribu na na heshimu pia haraka zao."

Pia Aslay ameongeza kuwa Tamasha hilo litakuwa la kipekee sana kutokana na ladha ya muziki utakaopigwa utakuwa wa vyombo  mubashara (LIVE) ambapo atatumia dakika 100 kwa Nyimbo 100 jukwaani.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...