Na Mwandishi wetu, Nzega

KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaibu Kaim ameipongeza kampuni ya ASHARIQ CONSTRUCTION COMPANY LIMITED kwa uwekezaji mkubwa wa mradi wa maduka 74 uliopo Mjini Nzega Mkoani Tabora.

Akizungumza leo jumatano September 20 Kaim wakati mwenge wa uhuru ukiweka jiwe la msingi kwenye mradi huo wa majengo ya maduka ya SHABOUT.

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka huu amesema uwekezaji wa mradi huo ni mkubwa na utaendelea kuukuza mji wa Nzega, utachochea maendeleo ya eneo hilo na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo.

"Rais wa Serikali ya awamu ya sita Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo tumieni fursa hii kuwekeza, tunatambua jitihada za mwekezaji huyu hivyo mbio za mwenge wa uhuru kwa heshima kubwa tunaridhia kuweka jiwe la msingi la jengo hili," amesema Kaim.

Mkurugenzi wa kampuni ya ASHARIQ CONSERVATION COMPANY LIMITED Rashed Shabout Said amesema mradi huo wa maduka 74 ulianza mwezi Februari 2023 na unatarajiwa kukamilika Machi 2024.

Rashed amesema hadi mradi huo utakapokamilika utagharimu kiasi cha shilingi 800,000,000 na hadi kufikia sasa umefikia asilimia 70 ya gharama za ujenzi kwa shilingi 560,000,000.

"Fedha hizo zimetokana na ujasiriamali katika kodi za biashara za maduka ya SHABOUT SHOPPING CENTRE na ukandarasi katika kampuni ya ujenzi," amesema.

Amesema faida ya ujenzi huo ni pamoja na kuunga mkono sera ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzitaka sekta binafsi kuwekeza ili kuongeza ajira ambapo wanatarajia kuajiri watumishi zaidi ya sita, watakaotoa huduma mbalimbali katika jengo hilo ingawa kwa sasa wakati ujenzi ukiendelea wameajiri vijana zaidi ya 15 ikiwa ni pamoja na wataalamu 3.

Amesema faida nyingine ya uwekezaji huo ni pamoja na kuufanya mji wa Nzega uvutie sambamba na kulipa tozo na kodi mbalimbali Serikalini.

"Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita kuruhusu uwekezaji kupitia sekta binafsi na kutia chachu kwa wawekezaji kutafuta mitaji," amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Lemeya Tukai amepongeza uwekezaji huo uliofanywa na kampuni ya ASHARIQ CONSERVATION COMPANY LIMITED kuwa utachochea maendeleo ya mji wa Nzega.

"Tunaomba ukague mradi huu na ikikupendeza tunaomba utuwekee jiwe la msingi, mwenge wa uhuru hoyeeee tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa," amesema DC Tukai.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...