Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa -2023 ndugu Abdullah Shaib Kaim amezindua Mradi wa Maji wa Kibaoni Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya na kusema kuwa anaishukru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji miradi mingi ya maendeleo ikiwemo miradi wa maji.
 
Pia, amewashukru wadau ambao wameweza kushirikiana na Serikali kwa kutekeleza mradi wa maji wa Kibaoni. 
 
Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa mradi huu wa Kibaoni umejengwa kwa lengo la kuhudumia wananchi wa vijiji viwili vya kibaoni na Ihani.

Hata hivyo katika kuhakikisha kuwa mradi huu unakuwa endelevu, wananchi waendelea kutunza vyanzo vya maji, miundombinu ya maji pamoja na mazingira kwa ujumla " amesema.

Sambamba na kuzindua kwa mradi huo, Mwenge wa uhuru wa Kitaifa-2023 umeweza kutembelea chanzo cha maji cha Itamboleo pamoja na kupanda miti rafiki kwa mazingira ili kuweza kuhifadhi na kulinda chanzo cha maji cha Itamboleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...