Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha


Umoja wa wanawake UWT Pichandege,Kibaha , mkoani Pwani umeanzisha mradi wa fulana ambao utawawezesha kujikwamua ili kuondokana na utegemezi.

Aidha wameweza kuongeza wanachama wapya 200 kupitia siasa na michezo.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo na uzinduzi wa Bonanza la Selina Koka , Mwenyekiti wa UWT Pichandege, Neema Macha alieleza wamejipanga kujiinua kiuchumi kwa kuanzisha vitega uchumi .

Neema alieleza, ilani ya Chama Cha Mapinduzi inaeleza kuhusu kujiimarisha kiuchumi na kuanzisha miradi,hivyo kwa mpango huo waliouanza utawaongezea kipato.

"Tumekuwa tukiwa tunaomba fedha za ujenzi ,fedha za kufanikisha shughuli mbalimbali lakini kwa kupitia miradi yetu wenyewe itatuondoa huko katika utegemezi tutakuwa tunatoa fedha katika akaunti yetu na kufanikisha mipango na shughuli zetu"

"Tunaupinga umaskini,na sisi wanawake ni Jeshi kubwa tukipambana, tukiwezeshwa tunaweza,tunamshukuru mama yetu,mlezi wetu Selina Koka kwa kuanzisha haya na sisi tunaamini tukiyaendeleza tutafika mbali kimaendeleo"alifafanua Neema.

Kwa upande wake,Katibu wa UWT Pichandege Pili Yahaya alitaja changamoto ya uhaba wa raslimali fedha, maji eneo la Lulanzi Hali inayosababisha wagonjwa wanaokuwepo hospital ya Lulanzi kupata shida,ukosefu wa kadi za UWT na fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi.

Awali Mwenyekiti wa UWT Kibaha Mjini, Elina Mgonja aliwasihi wanawake wasikate tamaa .

Mgonja alieleza kwamba ,jitihada ,Umoja na kuchapakazi itawasaidia kutimiza ndoto zao ili kujiimarisha kwenye Umoja wao wa wanawake Kata.

"Nampongeza mama Selina Koka kwa kuwashika mkono akinamama ,kukuza Siasa na michezo kwa kuwapa jezi na mipira maeneo mengi kwenye kata mbalimbali na matunda yanaonekana kwa kata ambazo zimesimamia mwanzo wake"alieleza Mgonja.

Mgeni rasmi wa uzinduzi huo, mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka aliongoza harambee ya uzinduzi wa mradi wa fulana kwa kutoa sh.Milioni Moja kwa kununua t-shirts mbili.

"Jambo linalogusa utekelezaji wa ilani,jambo linalogusa jamii na wanaCCM huwa lazima mimi Kama mbunge,CCM Wilaya tulikimbilie na tuwepo ,Hili UWT Pichandege mmefanya Jambo kubwa na ni utekelezaji wa ilani"aliwapongeza Koka.

Akizungumza kuhusu uzinduzi wa Bonanza anasisitiza ,Siasa na michezo kwani ni suala linaloshawishi watu kujiunga na Jumuiya na Chama na kulinda afya zetu.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...