Ligi ya Chama cha soka mkoa wa Pwani COREFA  inatarajiwa kuanza Oktoba 14 mwaka huu katika viwanja tofauti ambapo pamoja na mambo mengine Timu zisizopungua 16 zilizokidhi vigezo zitashiriki.

Ligi hiyo ya COREFA itahusisha timu zinazotoka ndani ya Mkoa wa Pwani na kwamba zote zinapaswa kuzingatia miongozo ,kanuni na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya ustawi wa mpira ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa timu zote zinazoshiriki zinakamilisha taratibu zote ndani ya muda muafaka.

Aidha Timu  zote zinazoshiriki ligi ya COREFA  zinapaswa kuhakikisha kwamba kila mchezaji anakuwa na cheti halali cha kuzaliwa na hivyo kuepuka vyeti vya kugushi kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imepoteza sifa ya kushiriki sambamba na kuchukuliwa hatua.

" Oktoba 14 mwaka huu tunakwenda kuanza Ligi ya Mkoa ,tunavikumbusha vilabu kukamilisha usajili mapema lakini pia kutuma taarifa sahihi za wachezaji wao ambao watacheza ili kuepuka usumbufu usiokuwa na sababu za msingi.

Aidha " muongozo ulishatoka mapema kwamba wachezaji ambao wanasifa ya kushiriki kwenye ligi hiyo ni wale wenye umri chini ya miaka 20, lakini pia lazima awenacheti cha kuzaliwa sahihi tofauti na hapo hatakuwa na sifa, kwahiyo ni vema mkajikagua wenyewe kwanza  na kujiridhisha ili kuepuka usumbufu hapo badae.

Aidha COREFA inavielekeza vilabu vyote kuajiri makocha ambao wanasifa ya ufundishaji kwa ngazi ya Diploma D sambamba na kusajiliwa na chama cha soka Mkoa Pwani.

" Tunafaham kuwa kunamakocha wengi sikuhizi lakini makocha ambao wanahitajika kufundisha ni wale waliosoma nakupata cheti walau chakuanzia ngazi ya Diploma D lakini pia awe amesajiliwa na COREFA huyu ndio ataruhusiwa kukaa kwenye benchi.

Tunaitaji kuwa na Ligi ya kisasa ndani ya mkoa wetu hivyo vilabu vyote mjikague na kurekebisha kasoro ambazo mtaziona lengo ni kuona kwamba wote tunakwenda njia moja kwa mafanikio makubwa na hivyo kuendana sambamba na kaulimbiu ya Pwani mpira utachezwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...