Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 04, 2023 ameshiriki sherehe za uapisho za Rais mteule wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa zilizofanyika katika uwanja wa Harare, Zimbabwe.

Mheshimiwa Rais Mteule Mnangagwa ameshinda  uchaguzi  huo kwa kura zaidi ya milioni 2.3 kati ya kura milioni 4.4 zilizopigwa sawa na asilimia 52.6 dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa ambaye alipata kura milioni 1.9 sawa na asilimia 44.

Ushindi huo unamfanya Mheshimiwa Mnangagwa kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha pili cha miaka mitano.

Mheshimiwa Majaliwa amemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho huo.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...