Na. WAF - Mtwara 

Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais   wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imejenga majengo ya huduma za dharura 128 na majengo ya Huduma za wagonjwa mahututi  78 kwa mwaka 2023 nchi nzima.

Dkt. Mollel ameeleza hayo leo  Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akisalimia  wananchi wa wilaya hiyo.

“Mwaka huu Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga majengo ya huduma za dharura 128 nchi nzima na majengo ya huduma za wagonjwa maututi  78 ili kusaidia wananchi kupata huduma hizo kwa urahisi”. Amesema Dkt. Mollel

Aidha, Dkt. Mollel amesema kuwa ujenzi wa majengo ya huduma  za dharura na huduma za wagonjwa maututi kwa mwaka huu ambapo sekta ya afya yote imepewa trilion 6.7

Dkt. Mollel ameongeza kuwa kwa Mwaka huu X-RAY za kisasa 199 zimenunuliwa na kusambaza  katika Hospitali kwa ajili ya kutoa  huduma kwa wananchi ambapo X-Ray moja ya kisasa  inagharimu kiasi cha shilingi Milion 500.

"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepunguza Rufaa za kwenda  nje ya nchi kwa kuwezesha  Sekta ya Afya kutoa huduma za Sikoseli katika Hospital ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma  na Hospitali ya Mifupa (MOI) iliyopo Jijini Dar es Salaam kwa kuwa na mashine yenye uwezo wa kufanya upasuaji wa unaondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kwa kupitia puani", ameeleza Dkt Mollel

Pia, Dkt. Mollel amesema kuwa mashine hiyo ya kufanya  upasuaji wa  unaondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kwa kupitia puani imegharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 21 hiyo ni ishara ya upendo wa Rais Dkt. Samia kwa watanzania katika kulinda  Afya za Watanzania wasipate adha ya huduma za Afya.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...