Na Humphrey Shao,Michuzi TV
Mwenyekiti wa bodi ya REA na TAWENI ,Mh Janet Mbene ametoa wito kwa wanawake wa Kigamboni kuacha kutumia mkaa na kuni na waanze kutumia Gesi na Mkaa mbadala hili kuweza kulinda mazingira.
MH Mbene amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika Wilaya ya Kigamboni wakati alipokuwa akizungumza na wanawake wajasilimali wa Wilaya hiyo.
"Matumizi ya mkaa mbadala ayaepukiki Kwani tunavyoendelea kutumia mkaa unaokatwa kwenye miti tunachangia sana kwa kiasi kikubwa kufanya uharibifu wa mazingira na kupelekea kuapata mabadiriko ya Tabia nchi" amesema Mh Mbene.
Ameongeza kuwa Matumizi ya kuni pia uchangia matatizo makubwa ya kiafya ikiwemo wanawake na Wasichana kupata tatizo la kutoa mimba na homa ya mapafu.
Ametaja kuwa Taweni imejipanga katika kumkomboa Mwanamke kiuchumi kwa kupitia vikundi hili waweze kuacha kutumia mkaa na kuni na waanze kutumia Gesi na mkaa Mbadala.
Ameongeza kuwa ni muda sasa wa kinamama kujifunza namna ya kubadilisha maisha kwa kujifunza kutumia Nishati mbadala hivyo wamama waache kujifunza kwani kujifunza ndio kila kitu.
Mwenyekiti wa bodi ya REA na Taweni Mh Janet Mbene Mbene akizungumza na wanawake wa KIGAMBONI ambao waliofika katika semina ya Matumizi ya Nishati Mbadala.
Mwenyekiti wa bodi ya REA na Taweni Mh Janet Mbene akionja moja ya chakula kilichopikwa na Nishati mbadala.Mwenyekiti wa bodi ya REA na Taweni Mh Janet Mbene akisindikizwa na wanawake wa Kigamboni kwenda jukwaani
Mkurugenzi Mtendaji wa Taweni Florance Masunga akizungumza na wanawake wa Wilaya ya Kigamboni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...