Na Pamela Mollel

MHIFADHI Mkuu anayesimamia Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Hapyness Kiemi amesema uwepo wa Mradi wa  Mbwamwitu na Faru ndani ya hifadhi hiyo umefanya idadi ya wageni kuongezeka kwa asilimia 100 kwa mwaka 2022/2023.

Kiemi  ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo hivi karibu ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea ongezeko la watalii katika hifadhi hiyo kutokana na uwepo wa wanyama hao adimu.

Amesema bado wana matarajio ya kuongezeka kwa  wageni hususan wageni wa ndani na ongezeko hilo pia limetokana na uwepo wa  filamu ya Royal Tour iliyozinduliwa na Mh.Rais.

“Hifadhi yetu bado ina matarajio ya kuwa na ongezeko la wageni hususan wageni wa ndani ambao wanakuja kutazama Faru na Mbwamwitu na katika kipindi cha miaka miwili ijayo tunatarajia wageni kuongezeka zaidi, "amefafanua Kiemi.

Kwa upande wake Mhifadhi Mwandamizi  anayesimamia miradi hiyo ya wanyama adimu Emanueli Sisya ameeleza kuwa  hifadhi ya Mkomazi ilichanguliwa kama hifadhi ya uzalishaji Mbwa mwitu kutokana na eneo hilo kushabihiana na mazingira  wanayoishi mbwa hao

Sisya  amefafanua kuwa mradi huo ulianza ukiwa na mbwa mwitu 25 ila kwa sasa wameongezeka na kufikia zaidi ya 300 ambapo huwaachia mbwa hao katika mifumo ya kiiolojia na kwa sasa  lengo lao ni kuzalisha na kuwarudisha katika maeneo yao ya asili

“Mbwamwitu ni wanyama wanaoishi kimakundi kwa maana ya kifamilia hivyo tunawaachia katika makundi tukiangalia mbwamwitu wenye umri unaolingana, amesema Sisya

Aidha amezitaja faida zinazotokana na mbwamwitu kuwa  ni kivutio kikubwa cha utalii hususan kwa  wageni  ambao wengi wamekuwa wakitembelea hifadhi hiyo kutokana na  uwepo  wa kivutio hicho cha mbwa mwitu,na hivyo wana mpango wa kuendelea kutanua kwa kujenga boma lingine ili kuwezesha wageni kuendelea kuwaona na utalii kukua

Kwa upande wake Mratibu wa Wanyama hao Jackson Lyimo amezitaja  changamoto kubwa wanazokabiliana nazo mbwamwitu  kuwa  ni pamoja  na  migongano baina ya wafugaji  na  wanyama hao kwa kuwa wanawaona kama wanyama waharibifu

Lyimo amefafanua  tangu  kuzalishwa kwa  mbwamwitu  katika hifadhi ya Mkomazi  tayari wameachia makundi 15 yenye mbwa zaidi 209 ikiwa ni kurudisha  ikolojia ya hifadhi ya  Mkomazi kwa kuwarudisha  katika hifadhi ambazo zilikuwa na mbwamwitu  ila wakatoweka kutokana na sababu mbalimbali

“Mbwa hawa pia wanakutana na changamoto za magonjwa pindi wanapokutana na wanyama wakufugwa lakini pia binadamu ni adui mkubwa wa wanyama hao kwa kuwa wanamuona kama mharibifu”.Alifafanua Lyimo.

Mradi wa mbwa mwitu katika hifadhi ya Mkomazi  ulianzishwa mwaka 1995 ukiwa na lengo la kuzalisha  mbwa mwitu na kuwarudisha katika maeneo yao ya awali kutokana na kuendelea kutoweka kutokana na sababu mbalimbali

 Jackson Lyimo,mratibu wa mradi wa Mbwa mwitu hifadhi ya Mkomazi akizungumza na vyombo vya habari hifadhi hapo

 Emanuel Sisya,Mhifadhi mwandamizi,hifadhi ya Mkomazi anayesimamia mradi wa wanyama Adimu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...