*Alia na changamoto ya migogoro ya ardhi, kuzuiwa kulima

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MGOMBEA ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Bahati Ndingo amekiomba Chama chake na serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuangalia upya changamoto ya migogoro ya ardhi iliyopo ndani ya wilaya hiyo.

Amesema asilimia zaidi ya 90 ya wananchi wa Wilaya ya Mbarali ni wakulima hivyo ardhi ndio maisha yao na ndio uchumi wao wanapozuiliwa kulima kwa sababu ya uwepo wa tangazo la GN 28 ni kurudisha nyuma uchumi na maendeleo yao.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za Chama hicho za ubunge katika jimbo hilo, Bahati ameeleza kwa kina kuhusu tangazo la GN 28 linavyoathiri maisha ya wananchi wa wilaya hiyo na kuomba ni vema likapitiwa upya.

“Migogoro ya ardhi ndio inafanya wilaya hii iwe nyuma. Unapotuona hapa zaidi ya asilimia 90 ni wakulima, linapokuja suala la ardhi sisi hatuitafuti kujengea maghorofa, hatutafuti ardhi kujenga nyumba.

“Suala la ardhi Mbarali sio la masihara, tunaangalia ardhi kama maisha yetu, kama uchumi wetu kwa sababu asilimia 90 ni wakulima. Nakushukuru Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine mmefika na mmeona changamoto iliyopo na mmeona ukubwa wa tatizo.

“Ujio wenu Mbarali kwa sasa tumeongeza mashahidi wa kututetea Mbarali, mwanzao wakati tunazungumza tulikuwa tunatafsiriwa tofauti. Naamini ndani ya CCM tuna uwezo wa kutafuta ufumbuzi, wana Mbarali na mimi mtoto wenu mniniamini, nilianza kuzungumza kabla na nitaendelea,” amesema.

Amefafanua kuwa Rais Dk. Samia hataki kuona migogoro ya ardhi ikiendelea na ameanza kuchukua hatua kwani vijiji 34 vilikuwa vinatakiwa kuondoka, lakini vijiji 29 tayari vimeruhusiwa na vijiji vitano ndivyo vilivyobaki.

Ndingo amesema vijiji vitano ambavyo vimebakia ndio vimebeba uchumi wa Mbarali na ndivyo vilivymebeba maisha ya wananchi wa wilaya hiyo na wapenda maendeleo.

“Tunaokuomba Makamu Mwenyekiti, tupitie jambo hili kwa maslahi ya wana Mbarali na wapenda maendeleo ambao uchumi wa nchi chakula kinatoka Mbarali

“Kutokana na mgogoro huu wa GN 28 kuna vijiji vimesitishiwa huduma, hata barabara kuchongewa imekuwa shida.Tunaomba Serikali itoe huduma kwa wananchi wote wa Mbarali."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...