Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mhe.Sebastian Waryuba amezindua zoezi la uwekaji wa vigingi vya mpaka wa Pori la Akiba Kilombero katika hafla iliyofanyika Septemba 11, 2023, Kilosa Mpepo, Mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo, Mhe. Waryuba alisema uwekaji wa vigingi hivi utasaidia kupunguza migogoro baina ya wananchi na wahifadhi iliyosababishwa na kukosekana kwa mipaka inayoonekana. Aidha, alitoa rai kwa wananchi ambao wameanzisha makazi ya muda ndani ya hifadhi waondoke bila kusubiri mkondo wa sheria dhidi yao.

Vilevile, Mhe.Waryuba aliongeza kuwa ni wakati sasa wa wananchi kuacha kuvamia maeneo ya hifadhi na kuanza kuharibu uoto wa asili kwa kukata miti ovyo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji.

Awali akiwasilisha taarifa hifadhi hiyo, Kamanda wa Uhifadhi wa Pori la Akiba Kilombero, Bigilamungu Kagoma aliwashukuru wananchi wa Kilosa Mpepo kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa TAWA, na alitoa rai kwa wananchi kuacha kuingia ndani ya hifadhi kwa ajili ya shughuli za kibinadamu na kushirikiana na Serikali katika kuhifadhi eneo hilo kwa manufaa ya vizazi vyote.

Pori la Akiba Kilombero lilianzishwa kwa tangazo la serikali (GN) Na. 64 ya tarehe 17/02/2023 chini ya Sheria ya Uhifadhi wa wanyamapori Sura 283 likiwa na ukubwa wa Kilomita za mraba (Km²) 6,989.3.






 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...