Na Mwandishi Wetu           

MTANZANIA  Alice Gyunda  ni miongoni mwa washiriki 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliofanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha taji la  miss /mrs africa shindano linalifanyika nchini Uingereza.   

Akizungumzia shindabo hilo Alice amesema amevutiwa kujiunga kwenye shindano hilo ambalo kuna vitu tofauti tofauti anatarajia kuvifanya.  

Ameongeza kuwa malengo yake kama watanzania watampigia kura na kushinda  ana mpango wa kuanzisha vituo vya kuibua vipaji kwa wasanii wa sanaa ya muziki kila mkoa 

Alice amesema kupitia vituo hivyo vya kuibua vipaji kwa watoto pia vitakuwa na mkakati endelevu wa kutunza wasanii watakaopatika katika vituo hivyo kwa kuwawezesha kupata taalum ya sanaa ya muziki.

Aidha amesema uanzishwaji wa vituo vya uibuaji vipaji vitakavyoanzishwa vitakamilika katika sekta zote za uwepo wa studio za kisasa kwa ajili ya kurekodi nyimbo ambapo pia kwa wasanii watakaofanya vizuri wataunganishwa kufanya muziki wa pamoja na wasanii wakubwa wa Tanzania,  Ulaya na Afrika.

Amesema lengo la kuanzisha vituo hivyo vya kuibua vipaji ni kutaka kuandaa wasanii wengi wakubwa wa muziki wa bongo flavor , hip poo, singeri na rage ili wawe kama walivyo  wasanii wakubwa kama akina Diamond, Ally Kiba Harmonize  na wengine wengi ambapo wakifanikiwa  Tanzania itakuwa na wasanii wakubwa chipukizi wa kuziba pengo hilo.

Shindano la Miss/Africa uk ni shindano linaloshirikisha waafrika wanaoishi nchini Uingereza ambao walifanikiwa kuingia baada ya kukidhi vigezo vya kuingia kwenye shindano hilo ambalo linaandaliwa na taasisi ya africauk pageants ya nchini Africa Kusini.

Tayari awamu ya kwanza ya mchujo imepita  na kupatikana warembo 20 watakaoingia kwenye tano bora hadi kupatikana mshindi wa kwanza hadi wa tatu kura yako na anasema ushindi wake nj ushindi wa watanzania anaomba kupigiwa kura.

Ushindi wa shindano hilo ni namna mshirika anavyopigiwa kura kupitia website ya https//afrikaukpageants. co. uk/poll/mrs-missafrica-finalist-2023.

Hata hivyo  bado nguvu ya watanzani kushiriki katika kumpigia kura Mtanzania huyu imekuwa ni ndugu tofauti na namna ya ushiriki wa taifa jirani la Uganda ambapo wanajitokeza kwa wingi kumpigia kura mshiriki wao.

Kutokana na changamoto hiyo mshiriki Alice gyunda amewaomba watanzania kutoka nchi mbali mbali kushiriki kumuunga mkono kwa kupimpigia kura nyingi za ndiyo kupitia link ilianishwa hapo juu ambapo mwisho wa kupiga kura ni Septemba 10.

Anasema ushindi wake ni fursa kwa watanzania ambapo kwa mujibu wa zawadi zilizoanishwa kwenye shindano hi pamoja na mshindi atakayetwaa taji hilo atapata fursa ya kuandika andiko la namna atakavyosaidia watoto wanaishi katika mazingira magumu katika nchi yake ya uraia.

Ameongeza  hadi sasa ni asilimia sita ya upigaji kura wa watanzania katika shindano hilo huku mshiriki wa Uganda akiongoza kwa asilimia 39 na kuwaacha  mbali washiriki wengine akiwamo mtanzania Alice Gyunda.

Pamoja na hayo Alice amesema tayari mtanzania huyo ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika mazingira  magumu katika Halmashauri ya Mkuranga.Msaada huo ni  unga, sabuni, mchele na mafuta ya kula.

Mtanzania Alice taalum yake ni ualimu na  kabla ya kwenda kuishi ughaibuni akiwa nchini Tanzania amewahi kufundisha Shule ya Msingi Kawe na Osterbay.Pia mshiriki huyo ni msanii anayeimba maudhui ya uelimishaji.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...