Na Albano Midelo,Songea

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amelitaja eneo lenye
fursa nyingi za uwekezaji Ruvuma kuwa ni sekta ya kilimo.

Akizungumza wakati anafungua kongamano la Biashara na Uwekezaji la
Mkoa kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea,Kanali Thomas ameyataja
mazao makuu ya biashara yanayozalishwa kuwa ni ,kahawa,korosho na
tumbaku.

Mazao ya chakula na biashara ameyataja kuwa ni
mahindi,ufuta,soya,mbaazi,alizeti,mpunga,maharage,tangawizi na mzao
mengine ya bustani.

“Mkoa wa Ruvuma ndiyo mzalishaji mkubwa wa kwanza wa mazao ya
nafaka nchini,hata hivyo lengo la Mkoa ni kuzalisha zaidi hivyo tunahitaji
uwekezaji kwenye viwanda vya mbolea na viuatilifu kwenye kilimo”,alisema
RC Thomas.

Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma umetenga maeneo ya uwekezaji
katika kilimo cha Pamoja yenye jumla ya hekta 25,017 ambazo
zimetambuliwa na zinatakiwa kuwekezwa.

Amesisitiza kuwa Mkoa wa Ruvuma una mazao ya kutosha kuanzisha
viwanda vya uchakataji ambapo kwa mwaka 2022/2022 Mkoa ulizalisha
tani 25,284.5 za korosho,tani 13,700 za kahawa,tani 7,970.2 za ufuta,tani
5,152.3 za soya,tani 2,846.9 za mbaazi na tani 731,224 za mahindi.

Amesema katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma
umezalishaji tani 1,598,163 za mazao ya chakula hali iliyosababisha Mkoa
kuwa na ziada ya chakula tani 1,043,525.

Ameutaja Mkoa wa Ruvuma kuwa una mabonde yanayofaa kwa kilimo cha
umwagiliaji na kwamba kuna jumla ya hekta 197,108.2 zonazofaa kwa
kilimo cha umwagiliaji ambapo hadi sasa ni hekta 7,388.3 tu
zilizoendelezwa sawa na asilimia 3.7.
Mkoa wa Ruvuma  Kanali Laban Thomas akizungumnza baada ya kufungua kongamano la  biashara na uwekezaji Mkoa wa Ruvuma lililofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka mkoani Ruvuma walioshiriki  kongamano la  biashara na uwekezaji Mkoa wa Ruvuma lililofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...