Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akipitia nyaraka mbalimbali wakati wa Kikao cha majumuisho kwa ujumbe wa Tanzania kilichofanyika kwenye bustani ya Cresta Mowana Hotel, kabla ya kuhudhuria Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu unaofanyika Mjini Kasare -Botswana. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na kulia ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Sauda Msemo.


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiongoza Kikao cha majumuisho kilichofanyika katika bustani ya Cresta Mowana hotel Mjini Kasane – Botswana, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu.


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), katikati (walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Tanzania uliohudhuria Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu, unaofanyika katika hotel ya Cresta Mowana, Kasane – Botswana. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb),akifuatilia baadhi ya matukio katika ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Cresta Mowana, nchini Botswana.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akifuatilia baadhi ya matukio katika ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu, unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Hotel ya Cresta Mowana, nchini Botswana.


Baadhi ya ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakifuatilia baadhi ya matukio katika ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu, unaofanyika katika Hoteli ya Cresta Mowana, nchini Botswana. (Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha-Botswana)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...