Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi limetembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha lengo likiwa ni kujionea vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ambayo inapatikana ndani ya mkoa wa Arusha sambamba na kuhamasisha watu kutembelea vivutio hivyo.

Akiongoza zoezi hilo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, CP Awadh Haji alisema wameona fahari kutembelea hifadhi hiyo yenye vivutio mbalimbali ikiwa ni kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais za kuutangaza utalii wa Nchi yetu.

CP Awadh alibainisha kuwa ziara hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha uhusiano, kutatua changamoto za kiusalama baina ya Jeshi hilo na wadau wengine wanaohusika moja kwa moja kuhudumia watalii.

Sambamba na hilo pia alisema Jeshi hilo limeingia mkataba wa mashirikiano na Chuo cha Taifa cha Utalii ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji Maafisa, Wakaguzi na Askari ili kuhakikisha wanakwenda kutoa huduma bora kwa watalii na wageni wote wanaofika nchini.

‘’Dhamira ya Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu ni kukuza Utalii wa nchi yetu na kuongezeka idadi ya watalii nchini, hivyo sisi Jeshi la Polisi tutahakikisha tunaenda kutoa huduma bora kwa watalii  na wageni wanaofika nchini sambamba na kuimarisha usalama wao. Alisisitiza CP Awadh.

Kwa upande wake Mhifadhi wa Hifadhi hiyo ACC Yusta Kiwango alisema wamekua na mahusiano mazuri na jeshi la Polisi ambapo mara nyingi hufanya operesheni za pamoja hali ambayo inapelekea Watalii wanaotembelea hifadhi hiyo kufurahia mandhari bila ya uwepo wa changamoto za kiusalama.

Aidha ametoa wito kwa taasisi nyingine za serikali na za binafsi kutembelea hifadhi hiyo ili kujionea vivutio vilivyopo sambamba na kuutangaza utalii wa Nchi yetu.

Ziara hiyo imekuja mara baada ya Jeshi hilo kuingia mkatabata wa mashirikiano na Chuo cha Taifa cha Utalii jana Jijini Arusha ambapo maafisa wa Jeshi hilo watajengewa uwezo wa kiutendaji wa namna bora ya kuwahudumia watalii.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...