WILAYA YA HANANG, (18/09/2023) - Serengeti Breweries Limited inafurahi kutangaza uzinduzi wa Programu ya “Learning for Life” kwa vijana wa Wilaya ya Hanang. Hatua hii inathibitisha dhamira ya Serengeti Breweries Limited ya kuwawezesha zaidi ya vijana 400 wa Hanang kupata ujuzi na maarifa muhimu kwa ajili ya maendeleo binafsi, ujasiriamali, usimamizi wa kifedha, na mipango bora ya biashara zao. Serengeti Breweries Limited inafuraha kutangaza kuwa program hii itaanza tarehe 18 Septemba 2023 na kumalizika tarehe 21 Septemba 2023.

Warsha ya Kujifunza kwa Maisha inakwenda sambamba kikamilifu na lengo la Wilaya ya Hanang la kutoa huduma bora na zilizo endelevu ifikapo mwaka 2025. Kwa kuwajengea vijana wetu ujuzi muhimu, tunachangia kwenye azma ya wilaya hii ya kuboresha huduma za kijamii na matumizi bora ya rasilimali.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Cuthbert Sendiga, alisema, "Nina furaha kuona Programu ya “Learning for Life” yakifanyika katika Wilaya ya Hanang. Hatua hii ni muhimu sana kwa mkoa wetu na inakwenda sambamba kikamilifu na lengo la Wilaya ya Hanang la kutoa huduma bora na zilzio endelevu ifikapo mwaka 2025. Hatua hii haitawawezesha tu vijana wetu bali pia itachangia ukuaji wa kiuchumi na maendeleo ya Wilaya ya Hanang. Itaunda kundi la watu wenye ujuzi na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya na uvumbuzi katika jamii yetu."

Tanzania inajivunia idadi kubwa ya vijana, takriban asilimia 64 ya jumla ya watu, lakini tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana linaendelea kuwa changamoto, na viwango vya asilimia 13.6 kwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 15-24. Upatikanaji mdogo wa mafunzo bora ya ujuzi unachangia tatizo hili, haswa katika Wilaya ya Hanang, ambapo vijana wanafanya karibu asilimia 70 ya idadi ya watu. Ni muhimu kutatua changamoto hii kwa dhati.

Programu ya “Learning for Life” unatoa nafasi ya kuwawezesha vijana kujiajiri na kujenga ajira. lengo kuu la Serengeti Breweries Limited ni kuwasaidia kutambua fursa na kuzitumia kwa ufanisi. Fursa hii inawawezesha vijana kutengeneza mtandao wa kijamii, kujifunza kutoka kwa wataalamu, na kupata ufahamu wa vitendo katika sekta mbalimbali, yote haya yakiwa na lengo la kupunguza ukosefu wa ajira, kupunguza umaskini, na kutengeneza fursa kwa vijana wa Wilaya ya Hanang.

Kwa mujibu wa Rispa Hatibu, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa Serengeti Breweries Limited, "Serengeti Breweries Limited inaamini kuwa kuwekeza kwa vijana ni kulinda mustakabali wa jamii yetu. Kupitia programu ya Kujifunza kwa Maisha, Serengeti Breweries Limited inatoa ujuzi na pia inakuza uwezo wa vijana wa Hanang kuwa viongozi, wajasiriamali, na wachangiaji katika ukuaji na mafanikio ya wilaya hii."
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...