Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan mapema leo hii Septemba 15, 2023 amezindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara.

Rais Samia amesema kuwa kukamilika kwa Hospitali hiyo ambayo ina watalaam, vifaa na vifaatiba vya kisasa itasaidia watu wa Kanda ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kupata uhakika wa huduma za matibabu ya kibingwa karibu na maeneo yao.

“Wagonjwa wote wenye matatizo makubwa watakuja hapa, jengo hili litumike kutoa huduma za afya” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema kuwa kazi ya watumishi wa afya ni kuokoa maisha ya watu hivyo watumishi hao wajitumie kufanya kazi kwa kuwa Serikali imewekeza kwenye miundombinu, vifaa na dawa na wao watimize wajibu wao

Tunahitaji matunzo ya jengo hili, vifaa na huduma kwa wananchi kwa lugha nzuri, kila mtu amepangiwa jukumu lake na Mwenyezi Mungu, tumridhishe Mungu kwa huduma tunazozitoa, nawatakia kila la kheri” amesema Rais Samia huku akiongezea kuwa changamoto zilizopo za watumishi zitaendelea kufanyiwa kazi kwa haraka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...