Na Mwandishi wetu

MKUU  wa Mkoa wa Geita Martin Shigella ameishauri kampuni ya Al mansour Tanzania ambao ni wauzaji na wasambazaji wa magari aina ya ISUZU kuchangamkia fursa zinazopatikana kanda ya Ziwa.

Fursa hizo ni katika sekta ya madini kwa kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za madini yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni katika mkoani humo.

Akizungumza jijjini Dar salaam  hivi karibuni alipotembelea ofisi ya Kampuni ya ISUZU, Shigella amesema ni muhimu kampuni ya Al mansour Tanzania  kuchangamkia fursa lukuki zinazopatikana kanda ya Ziwa kwa sasa.

"Niwaombe Al mansour Tanzania muanza kuchangamkia fursa zinazopatikana ndani ya Mkoa wa Geita,mojawapo kubwa ni hii ya kushiriki maonesho ya Kimataifa ya bidhaa za madini yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni '',amesema Shigella.

Ameongeza  lengo la kuwahamasisha ushiriki wa maonesho hayo,ni kuona na wao wanaitumia fursa hiyo kutanua wigo wa biashara zao,kukutana na wafanyabiashara wapya ikiwemo na hata kubadilishana mawazo katika suala zima la uwekezaji katika maeneo mbalimbali .

Amesema kwa kufanya hivyo pia watakutana na wadau walioko katika sekta za madini ukanda huu wa Afrika Mashariki,wakiwa na bidhaa/magari yao kuyatangaza zaidi na kuwa na soko la uhakika kanda ya ziwa.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini Tanzania Anurup Chatterjee amesema ni faraja kwao kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, wao wanathamini jitihada zilizowekwa na serikali kuhakikisha maonesho yanafanikiwa na kuleta tija.

"Sisi kama kampuni ya Magari ya ISUZU tunawahakikishia  wateja wa Kanda ya Ziwa wasipate usumbufu, tumedhamiria kushiriki maonyesho hayo ukizingatia mwaliko alioutoa Mkuu wa Mkoa,kwetu sisi ni maagizo hivyo hatutomwangusha'',amesema Chatterjee

Amesisitiza atahakikisha timu mzima ya mauzo inaweka kambi kanda ya ziwa kwa kipindi chote

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigella akipokea zawadi kutoka kwa Country General Manager wa kampuni ya Almansour Auto Ltd ,wauzaji wa magari ya Isuzu wakati mkuu huyo wa mkoa alipotembelea ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es salaam ikiwa ni ziara ya kuhamasisha ushiriki wa maonyesho ya madini ya Geita yatakayofanyika hivi karibuni.Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe Martin Shigella na Country General Manager wa kampuni ya Almansour Auto Ltd ,wauzaji wa magari ya Isuzu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi

 Mkuu wa Mkoa Mhe.Shigella akitembelea ofisi za kampuni ya Isuzu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...