Mkuu  wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika jana mkoani hapa. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk. Fatma Mganga.

.............................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameziagiza Halmashauri kuhimarisha ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha mashine za kukusanya fedha ] POSS} zisitumike feki.

Serukamba alitoa maagizo hayo wakati akizungumza na wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri na wataalam mbalimbali katika kikao kazi kilichofanyika jana mjini hapa.

Alisema kumekuwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato na matumizi ya POSS feki hivyo kuukosesha mkoa kupata mapato stahiki ambapo aliviomba vyombo vya dola ikiwamo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa} TAKUKURU } kusaidia kufanya uchunguzi kwenye mageti ya ukaguzi wa mazao yanayosafirishwa.

Aidha, Serukamba alisema Mkoa wa Singida unaweza ukawa kinara wa ukusanyaji wa mapato, uhifadhi wa mazingira na usimamizi wa miradi iwapo tu watendaji watafanya kazi kwa kujituma na kushirikiana badala ya kuyaachia baadhi ya makundi kufanya kazi hizo.

'' Tukifanya kazi vizuri katika uhifadhi wa mazingira, ukusanyaji mapato, ukamilishaji wa miradi kwa wakati na kuwa timu moja, siku moja  tutakuwa namba moja kitaifa,'' alisema Serukamba.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk.Fatma Mganga akizungumza kwenye kikao hicho aliwaomba wakurugenzi pindi wanapopokea fedha za miradi kabla ya kuanza kutekelezwa watoke ofisini na kwenda kujua bei za vifaa badala ya kwaachia watu wa manunuzi pekee ambao wamekuwa na changamoto ya kuweka bei ya juu.

'' Miradi mingi imekuwa haikamiliki kutokana na fedha zilizotolewa na Serikali kumalizika kabla haijaisha na hiyo inasabishwa kununua vifaa kwa bei kubwa lakini wakurugenzi wakitoka na timu yao watawakuta wauzaji wa vifaa hivyo kwa bei ya chini.'' alisema Mganga.

Mganga akitolea mfano alisema alipokuwa mkurugenzi wa halmashauri wakati wanataka kutegeneza milango waliwaomba watu wa manunuzi wawape bei yao ambapo wasema ni Sh.Milioni 72 na walipotoka kutafuta bei kwa watu wengine alikuwepo wa Sh.Milioni 50 na mwingine Sh.Milioni 48 na hivyo kumpa kazi hiyo aliyekuwa na bei ya chini ambaye alifanya kazi hiyo kwa viwango vya hali ya juu.

Katika hatua nyingine Mganga aliwaomba wakurugenzi hao kujenga tabia ya kwenda kujifunza kwa wenzao ambao wanafakiwa kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati na kwa fedha zilezile walizopokea kama wao.

Alisema utakuta Serikali imetoa fedha kiwango sawa lakini katika ukamilishaji wa miradi kwa fedha hizo hizo halmashauri zingine zinakamilisha miradi iwe ya ujenzi wa shule au vituo vya afya na halmashauri nyingine utakuta ujenzi wake upo hatua ya msingi.

Aidha, Mganga aliwahimiza watendaji hao kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kabla ya Agosti 9, 2023 ambapo ndio itakuwa kikomo cha fedha za bakaa na baada ya hapo zitarudi Serikalini.

Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine wakurugenzi na wakuu wa wilaya walitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato na miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye wilaya zao.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akizungumza kwenye kikao hicho.
Wenyeviti wa Halmashauri wakiwa kwenye kikao hicho.
Wakuu wa Wilaya wakiwa kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Jumanne Mlagaza, akichangia jambo kwenye kikao hicho. 
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi,  John Mgalula, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda  akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili akichangia jambo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula akiwa kwenye kikao hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...