Wakala wa nishati vijijini REA imefanya ziara mkoani Pwani kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo ya vijijini ili kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na kupunguza uhalibifu wa mazingira.

Akizungumza baada ya kupitia miradi hiyo,Mjumbe wa Bodi ya REA ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya fedha na Utawala Bw. Frolen Haule amesema Rea inakusudia kutekeleza lengo la serikali la kuhakikisha tasisi zote kubwa zinazotumia nishati ya mkaa kama chanzo cha nishati zinabadilika na kutumia nishati mbadala ifikapo january 2024, ili kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Haule ameendelea kusisitiza kuwa REA itaendelea kuziunga mkono tasisi ambazo zinajishughulisha na uzalishaji wa nishati mbadala ili kuuunga mkono juhudi za serikali la kuboresha mazingira za wafanya biashara na wabunifu wa nishati hizo.

Moja ya mradi uliotembelewa na ujumbe huo ni mradiwa kuzalisha majiko yanayotumia mkaa mbadala pamoja na majiko makubwa ya gesi chini ya kampuni ya Tango amabo umebeba dhima ya serikali ya kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa hasa maeneo ya vijijini.

Katika hatua nyingine Bw. Haule amewataka  wabunifu wa nishati mbadala kuzingatia taratibu zote za kiusalama ili kupunguza madhara ya kiafya yanayosababishwa na matumizi ya nishati hiyo wakati wa kupikia

Katika kupambana na uharibifu wa mazingira Serikali ilikuja na azimio la kutokomeza nishati ya mkaa na kuni ifikapo January 2024 ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na uchafuzi wa anga pamoja na kusababisha jangwa kwa  ukataji miti ovyo kwa ajili ya mkaa wa kupikia majumbani pamoja na taasisi mbalimbali

Kwa upande wake Gabriel kushoka Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kuja na Kushoka tools man manufacture Ltd,  Zinga Bagamoyo alisema kuwa kutokana na maelekezo ya Serikali yaliyotolewa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan, wetu kuwa watu waanze kutumia mkaa mbadala, hivyo kiwanda cha Kuja na Kushoka kimeshiriki kutekeleza agizo la serikali kwa vitendo kwa kuwekeza kwenye utengenezaji wa mkaa mbadala.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...