Afisa Elimu Mwandamizi toka Wizara ya Elimu, Bi. Hawa Juma Selemani (wa tatu kulia) aliyemwakilisha Kamishna wa Elimu Tanzania akizinduwa rasmi nembo mpya ya Shirika la Room to Read Tanzania kwenye Kongamano la Usomaji lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Room to Read Tanzania, Bw. Juvenalius Kuruletera pamoja na wageni meza kuu wakishuhudia tukio hilo.

Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mwandamizi toka Wizara ya Elimu, Bi. Hawa Juma Selemani (wa pili kushoto) pamoja na wageni wengine meza kuu kwenye Kongamano la Usomaji wakitembelea mfano wa maonesho ya maktaba toka Room to Read Tanzania.

Mwandishi wa kitabu cha Mabala the Farmer, Bw. Richard Mabal akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Usomaji lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano la Usomaji.

Mkurugenzi Mkaazi wa Room to Read Tanzania, Bw. Juvenalius Kuruletera akizungumza kwenye Kongamano la Usomaji lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Afisa Elimu Mwandamizi toka Wizara ya Elimu, Bi. Hawa Juma Selemani (kushoto) aliyemwakilisha Kamishna wa Elimu Tanzania akizungumza kwenye Kongamano la Usomaji lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Room to Read Tanzania, Bw. Juvenalius Kuruletera pamoja na wageni meza kuu wakimsikiliza kwa makini.

Afisa Elimu Mwandamizi toka Wizara ya Elimu, Bi. Hawa Juma Selemani (wa tatu kulia) aliyemwakilisha Kamishna wa Elimu Tanzania akizinduwa rasmi nembo mpya ya Shirika la Room to Read Tanzania kwenye Kongamano la Usomaji lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Room to Read Tanzania, Bw. Juvenalius Kuruletera pamoja na wageni meza kuu wakishuhudia tukio hilo.

SHIRIKA la Room to Read Tanzania limezinduwa nembo mpya ikiwa ni  jitihada za shirika katika kuendana na mabadiliko yanayotokana na kukua kwa shirika na kupanuka kwa miradi inayotekelezwa na shirika. Uzinduzi rasmi wa nembo hiyo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mlimani City sambamba na maadhimisho ya Kongamano la Usomaji chini ya mgeni rasmi, Afisa Elimu Mwandamizi toka Wizara ya Elimu , Bi. Hawa Juma Selemani aliyemwakilisha Kamishna wa Elimu Tanzania.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Bi. Hawa Selemani alisema Kongamano la Usomaji ni matokeo ya tamko la shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (UNESCO) lililotolewa tarehe 26 Oktoba 1966, hivyo lina lengo la kukumbusha umuhimu wa usomaji kama kigezo muhimu cha kuheshimu na kudumisha utu na haki za binadamu. 

"...Siku ya Usomaji huleta jamii pamoja katika kujadili changamoto mbalimbali zinazochangia kutokujua kusoma na kuandika katika maeneo yao. Siku hii huangazia ukweli kwamba, bado kuna mamilioni ya watu ambao hawajui kusoma na kuandika hata leo, na wapo pia mamilioni wasiokuwa na tabia ya usomaji. Aidha, siku hii hulenga kujenga uelewa wa pamoja kwenye jamii kuhusu umuhimu wa kujua kusoma na kuandika ambao ndio msingi wa tabia ya usomaji na ujifunzaji," alisema kiongozi huyo.

"...Kama tunavyofahamu kwamba, usomaji ni uwezo wa kusimbua na kuelewa matini, hivyo, ni muhimu kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji wa KKK tukiwa tunalenga kujenga stadi za usomaji kwa wanafunzi wa shule za msingi. Mwanafunzi anapokua darasa la kwanza na la pili hujifunza stadi za kusoma na kuandika darasani. Hata hivyo, kujua kusoma na kuandika pekee hakutoshelezi kumfanya mwanafunzi kuwa msomaji mahiri na mwenye kupenda kujisomea. 

Hivyo basi, mwanafunzi huhitaji kupata fursa ya kujisomea vitabu kwenye maktaba ili kukuza stadi ya usomaji na kujenga tabia ya usomaji. Hii inamaanisha kwamba, mwanafunzi apate vitabu vya hadithi vinavyomvutia kupenda kujisomea, lakini pia kusikiliza hadithi kutoka kwa mwalimu ili kujifunza na kuiga usomaji fasaha. Aidha, maktaba hutoa fursa kwa mwanafunzi kusoma mara kwa mara, kusoma kwa hiari na kusoma kwa kufurahia na hatimaye huwa msomaji wa kujitegemea. Alifafanua Bi. Hawa Selemani.

Naye Mkurugenzi Mkaazi, wa Shirika la Room to Read Tanzania, Mkurugenzi Mkaazi wa Room to Read Tanzania, Bw. Juvenalius Kuruletera akizungumzia mabadiliko ya nembo ya shirika hilo amesema nembo ya awali ilitengenezwa kitambo kukiwa na mradi wa Usomaji na maktaba pekee, hivyo wameboresha ili kuhusisha Mradi wa Elimu kwa Msichana kwa kuwa sasa tuna miradi mikuu miwili; yaani Mradi wa Usomaji na Maktaba na Mradi wa Elimu kwa Msichana na Usawa wa Kijinsia.

"..Room to Read tumeboresha nembo yetu ili kuendana na mabadiliko yanayotokana na kukua kwa shirika na kupanuka kwa miradi. Yafuatayo ni malengo ya mabadiliko haya: Tumefanya maboresho ili kuyapa uzito ulio sawa maeneo yote ya miradi yetu kadri shirika linavyozidi kukua, Kuonesha msisitizo zaidi unaoakisi dira yetu ya sasa na ya baadaye pamoja na Kuboresha mwonekano kwa kuwa tangu mwaka 2016 hawajawahi kubadili nembo hiyo.

Aidha aliongeza kuwa Room to Read inatambua juhudi za serikali katika kutambua umuhimu wa kukuza tabia ya usomaji, kwani wameendelea kupeleka vitabu vya hadithi za watoto katika shule za msingi, hivyo ni muda muafaka sasa kupitia serikali na wadau mbalimbali wa elimu, kuanzisha maktaba kwenye shule zote za msingi ili vitabu hivyo viwekwe kwenye mpangilio maalumu na rafiki kwa watoto kuweza kuvifikia na kuviazima ili kujisomea. 

Room to Read iko tayari kushirikiana na serikali kupitia Wizara ya Elimu na Taasisi ya Elimu Tanzania katika kutoa ushauri wa kiufundi (technical support) juu ya usimamizi na uendeshaji wa maktaba hizo endapo serikali itakuwa imezianzisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...