Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ni mambo muhimu kwa nchi zinazoendelea hasa katika masuala ya uchumi wa kijamii kwa vile nchi hizo zinaweza kubadili maisha ya watu wake kupitia sekta muhimu kama ya kilimo, nishati na elimu.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipohutubia katika Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Kundi la 77 pamoja na China akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan unaofanyika katika ukumbi wa mkutano, Havana Cuba.

Aidha Mhe. Dk. Mwinyi amekumbusha namna nchi zinazoendelea zilivyoathirika vibaya na janga la maradhi ya UVIKO-19, kwa kupanda kwa bidhaa, mizozo ya kisiasa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema hizo ni baadhi ya changamoto zilizosababisha kupanda kwa gharama za maisha na kudhoofisha jitahada za kujikwamua kiuchumi kwa nchi zinazoendelea.

Katika hotuba yake alikumbushia namna nchi zilizoendelea zilivyobaniwa teknolojia ya kutengeneza chanjo nchi za mataifa ya kusini na kuzinyima kabisa msaada wa kiteknolojia ili ziweze kutengeneza chanjo, hali hiyo iliyosababisha makampuni ya utengenezaji dawa ya mataifa tajiri kujipatia faida kubwa kwa kuziuzia nchi masikini chanjo ya UVIKO-19.

Rais Dk Hussein Ali Mwinyi akazitanabahisha nchi za kundi la G77 na China wachukulie hayo yote kama somo na zisibweteke kusubiri msaada kutoka mataifa tajiri, huu ndio wakati wa kusema imetosha.

📍Havana , Cuba.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...