Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SERIKALI kupitia Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA amesema wanathamini na kutambua mchango wa mashindano ya Ndondo Cup katika maendeleo ya soka la Tanzania.

Mwinjuma ametoa kauli hiyo leo katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa fainali ya mashindano ya Ndondo CUP ambapo timu ya Madenge imeibuka bingwa wa mashindano hayo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga timu ya Kibangu Rangers mabao 2-0.

Akielezea zaidi kuhusu mashindano ya Ndondo Cup ambayo mwaka huu yametimiza miaka 10, Naibu Waziri Mwinjuma amesema kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kueeleza kuwa anafuatilia mashindano hayo inatoa picha halisi ya kubwa wa mashindano hayo.

“Nchi hii iko chini ya Amir Jeshi Mkuu Dk.Samia Suluhu Hassan sasa akisema anaangalia na ni shabiki wa Ndondo Cup shughuli nzima imebadilika na hili sio jambo dogo tena na mimi mwenywe nilishangaa Rais anaweza kuangalia Ndondo Cup lakini anakwambia vitu ambavyo vinaonesha kabisa yeye ni mfuatiliaji

“Hivyo inakupa picha moja tu haya ni mashindano ya msingi na yanatakiwa kutuliwa mkazo kwa ajili ya maendeleo ya soka la Tanzania,”amesema Naibu Waziri Mwinjuma.

Akitoa tathimini yake kwa miaka ijayo kutokana na uwepo wa mashindano kama Ndondo Cup ambayo yamekuwa yakiibua vipaji vya vijana wengi, amesema anaamini wachezaji wengi wa timu ya Taifa na Ligi Kuu au ligi daraja la kwanza wamepita kwenye mashindano kama hayo.

“Mashindano kama haya yanasadiia tu sio kuwandaa lakini kuwapa nafasi ya wachezaji kupata uzoefu wa kushindana lakini wanatulelea vipaji.Kwa hiyo taaswira inaonekana vizuri kwa kuwa muda mrefu hatuna mashindano ya ngazi za chini yenye urasmi kama huu.

“Kwa hiyo unapokuja urasmi hata skauti wanaweza kupita huku na tukapata wachezaji wazuri kwa ajili ya ligi zetu,”amesema na kuongeza kuwa suala la kuibua vipaji vya wachezaji vijana sio la mtu mmoja , ni jukumu la wote.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...