Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba ameshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Elimu na Maendeleo unaofanyika nchini Uingereza kuanzia tarehe 12 - 14 Septemba, 2023. 

 Mkutano huu unajulikana kama UKFIET International Conference on Education and Development.  

Katika Mkutano huo Dkt. Komba  ameshirikiana na  Bi. Joan  Minja kuwasilisha kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo katika maeneo ya msawazo wa walimu na usambazaji wa vitabu vya Kiada na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia. 

 Aidha, mkutano huo umehudhuriwa pia na Dkt. Charles Msonde Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bwana .Kayode Sanni Kiongozi wa Timu Mradi wa Shule Bora na Bwana.Benjamini Oganga,Kiongozi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Elimu(System Strengthening Lead).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...