Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, Mhe. Simai Sadiki wakati Kamati hiyo ilipopewa Semina ya Shughuli zinazofanywa na Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

 Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, kuhusu Shughuli zinazofanywa na Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), wakati kamati hiyo ilipokutana  jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, Mhe. Simai Sadiki.

 

Baadhi  ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo wakifuatilia Semina ya Shughuli zinazofanywa na Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), iliyowasilishwa kwao na Kaimu Mkurugenzi Mkuu  Bw.   Nelson Mlali, jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), Nelson Mlali akifafanua  jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo (hawapo pichani), kuhusu mapato yanayokusanywa na wakala huo wakati Kamati hiyo ilipopewa Semina ya Shughuli za Shirika hilo, jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), Nahodha Mussa Mandia akifafanua  jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo kuhusu shughuli zinazofanywa na Shirika hilo wakati Kamati hiyo ilipopewa Semina ya Shughuli za Shirika hilo, jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

 

PICHA NA WIZARA YA UCHUKUZI





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...