Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Thomas Malekela amesema Tume imejipanga kuanzisha kanuni ya upatikanaji wa vyanzo vya mapato kwenye mashauri ya utatuzi wa migogoro ya kikazi.
Mhe. Malekela ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya Tume hiyo kwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo wakati wa kikao kazi cha kujadili kazi za Wizara pamoja na Taasisi zilizopo chini yake kilichofanyika Septemba 7, 2023 katika jengo la OSHA Jijini Dodoma.
Amesema ukusanyaji wa fedha hizo zitasaidia kwenye shughuli za maendeleo ya jamii na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.


Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Thomas Malekela akiwasilisha taarifa ya shughuri zinazofanywa na Tume kwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu wakati wa kikao kazi cha kujadili kazi za Ofisi hiyo na Taasisi zilizo chini yake kilichofanyika Septemba 7, 2023 katika jengo la OSHA Jijini Dodoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...