Madereva waliokuwa wakishiriki mafunzo ya muda mfupi chini ya walimu kutoka chuo cha VETA Mbeya wamewatakiwa kutii sheria za usalama barabarani na kuheshimu watumiaji wengine wa barabara ili kupunguza na kuondokana ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.

Hayo yamesemwa leo Septemba 21, 2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi Benjamin E.Kuzaga wakati akifunga mafunzo ya muda mfupi kwa Madereva wa magari ya Serikali, Makampuni binafsi, Malori waendesha mitambo. 

Kamanda Kuzaga amewataka madereva hao kwenda kuyaishi yale yote waliyofundishwa katika kozi hiyo ya muda mfupi yenye lengo la kuwajengea weledi katika uendeshaji vyombo vya moto na kuwajengea uwezo katika kujua sheria, kanuni na alama za usalama barabarani.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya Mhandisi Rajabu Ghuliku amesisitiza madereva wahitimu kuwa na udereva wa kujihami kwa kipindi chote wanapokuwa barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Mafunzo hayo yalianza Julai mosi, 2023 ambapo Jumla ya madereva 82 wamefanikiwa kuhitimu mafunzo hayo na kutunukiwa vyeti vya Udereva chini ya usimamizi wa wakufunzi kutoka VETA Mbeya.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya na Chuo cha VETA linaendelea kutoa elimu kwa madereva ili kudhibiti ajali za barabarani. 

Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga vizuri kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea maadhimisho ya sherehe za watu wenye uoni hafifu na usikivu hafifu ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Mbeya kuanzia Septemba 27, 2023 na kilele chake kufanyika Septemba 30, 2023 katika uwanja wa Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...