Njombe
Jamii nchini imetakiwa kuendelea kuwakumbuka watu wenye uhitaji kwa kutoa msaada wa vitu mbali mbali ili kusaidiana na kutatua changamoto ambazo watu wakiwemo wazee kwenye jamii wameendelea kukabiliana nazo.
Wito huo umetolewa na baadhi ya vijana wazawa wa kijiji cha Igola kilichopo mjini Njombe akiwemo Feliki Mwalongo na Basilisa Mwalongo walipokwenda kumtembelea Bibi Rainfrida Mgaya ambaye ni mkazi wa kijiji hicho mwenye umri wa zaidi ya miaka 100.
"Nitoe wito kwa vijana wenzangu kwamba warudi nyumbani wawasaidie wazazi kwasababu tunakosa baraka wakati mwingine kwasababu ya umimi"alisema Feliki Mwalongo
Stephano Msemwa ni mwenyekiti wa kundi la Njilikwa Fans (Marafiki wa Njilikwa) amesema kupitia wananchama waliopo kwenye kundi hilo wamefanikiwa kutoa msaada wa vitu mbalibali ikiwemo godoro ili kumsaidia bibi huyo anapopumzika.
"Siku ya leo kwa huyu bibi tumekuja kutoa msaada wa godoro,chumvi,sabuni lakini pia hata tochi kwasababu vitu kama hivi tunajua bibi anauhitaji mkubwa"alisema Msemwa
Bibi Rainfrida Mgaya ameshukuru vijana hao kwa kumsaidia kwa kuwa amekuwa akiendelea kuishi kwa kupata msaada kutoka kwa watu mbali mbali kutokana na umri wake.
"Ninashukuru sana na Mungu awabariki muendelee kunilinda"alisema Bibi Rainfrida Mgaya kwa lugha ya kibena
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...