Na. WAF - Dodoma

Wizara ya Afya kupitia Idara ya Tiba imetoa mafunzo ya ugonjwa wa Sikoseli kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma zaidi ya vyombo 40 kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kupata uelewa na kuweza kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa huo.

Hayo ameyasema leo Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Dkt. Caroline Damian wakati akifungua semina kwa waandishi wa habari juu ya ugonjwa wa Sikoseli iliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.

“Mwezi wa Tisa ulimwenguni kote tunazimisha mwezi wa uelewa wa Sikoseli kwa jamii, hivyo tumeanza kutoa elimu kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma zaidi ya vyombo 40 ili waweze kusaidia kuielimisha Jamii juu ya ugonjwa huo”. Amesema Dkt. Caroline

Aidha, Dkt. Caroline amesema kuwa mchango wa waandishi wa habari ni mkubwa sana Katika kuwafikia wananchi hivyo wataweza kuwafikia Watanzania wengi zaidi kwa kuwapa elimu juu ugonjwa huo wa Sikoseli ili kupunguza tatizo hili hapa nchini.

“Tunaamini kwamba waandishi wakielewa vizuri watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujibu maswali na kutoa elimu kwa Jamii ya kutosha”. Amesema Dkt. Caroline

Pia, Dkt. Caroline amesema kuwa kuna dhana potofu nyingi katika jamii kuhusiana na ugonjwa wa Sikoseli kwa sababu ni ugonjwa wa kurithi hivyo waandishi wa habari ni kundi muhimu sana litakaloweza kwenda kutoa elimu kwa jamii waondokane na dhana potofu hiyo.

Hata hivyo Dkt. Caroline ameiasa Jamii kupata elimu sahihi juu ya ugonjwa huo wa Sikoseli ambapo itawawezesha wasimamia Sera ya Afya kuweza kuwapata Watoto waliopo kwenye Jamii wenye ugonjwa huo ili waweze kupatikana matibabu sahihi.

“Jamii ikipata uelewa vizuri ambao ni sahihi itawezesha kuondokana na dhana potofu ambapo inapelekea wengine kuwaficha watoto wao hivyo itasaidia kupatikana kwa watoto wenye tatizo hilo na kuwapatia tiba sahihi sababu ukiwa na ugonjwa wa Sikoseli unaouwezekano mkubwa wa kupona”. Amesema Dkt. Caroline
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...