Na  Mary Margwe, Geita

 Wachimbaji wa madini na wanafanyakazi  katika maeneo ya uchimbaji wapo katika hatari ya kupata maradhi ya moyo kama hawatazingatia misingi kwa ajili ya afya kama kufanya mazoezi.

Akizungumza na waandishi wa habari Daktari bingwa wa Magonjwa ya moyo Dr.Salehe Mwinchete amesema  katika maonyesho ya madini hayo wamepeleka kliniki maalum inaitwa V.I.P Clinic ambayo ni kliniki ya watu mashuhuri lakini kweo sio watu mashauhuri wenye pesa, Bali  hiyo kliniki ni kwa kila mtu mwenye uhitaji wa huduma hiyo.

Wachimbaji hao wametakiwa kuhakikisha wanachukua tafadhari mbalimbali kuhakikisha kwamba kemikali zinazotumika katika kuchimba na kuandaa Madini waweze kuzingatia tafadhari.

" Watu wanaofanya kazi katika maeneo ya uchimbaji ni watu kama watu wengine, lakini wapo katika hatari ya kupata maradhi ya moyo kama hawatazingatia misingi Kwa ajili ya Afya kama kufanya mazoezi kwasababu mwisho wa siku mgonjwa anaweza kuharibu figo, lakini pia zikaenda hata kuharibu Moyo" amesema Dkt. Miwinchete.

Dkt. Mwinchete amesema " Naweza nikakuhakikishia kwamba Kemikali mbalimbali zinazotumika katika uchimbaji wa Madini Bahati nzuri hazina  madhara ya moja kwa Moja"

" Wito Kwa wadau wote wanaohusika katika maandalizi ya mchakato wa kuyapata madini wazingatie kemikali ambazo zinaweza kuleta athari katika mwili wa binadamu, zinazoweza kuleta katika Moyo japokua athari  sio ya Moja kwa Moja" amesema Dkt.Mwinchete.

DKt. Mwinchete amesema TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeleta kliniki ya maalum"V.I.P" ya huduma ya magonjwa ya moyo,Kliniki hiyo maalum inapatikana katika maonyesho ya sita(6) ya madini yanayofanyika kuanzia tarehe 20 september mpaka 30 September mwaka katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

Aidha,Dkt Salehe amefafanua jinsi kliniki hiyo inavyotoa huduma alisema "Mtu ataomba siku na muda ambayo anataka kuja kuhudumiwa katika kliniki maalum, atukutana na mazingira mazuri ya huduma,atafanyiwa huduma zote hapo hapo alipo kwa maana atamuona daktari hapo hapo,atapata vipimo hapo hapo na pia atapatiwa kiburudisho cha chai akiwa anasubiria majibu"

Pia Dkt Salehe ameelezea vyanzo tofauti tofauti vya maradhi ya moyo alisema kuwa ni ulevi,uvutaji wa sigara,matumizi ya chumvi nyingi katika chakula hivyo ameitaka na kuhihasa jamii kupunguza matumizi ya sigara na pombe ili kuepukana na maradhi ya moyo.

Pamoja na majukumu makubwa ya Taasisi ya Jakaya Kikwete Kwa matatizo ya moyo tunaelimisha, na kujenga uwezo kwa Wataalam mbalimbali kwa maradhi ya moyo.

Dkt. Mwinchete amesema  Mwitikio ni mkubwa sana kwasababu tunatoa huduma zilizobora sana, tunawapa Elimu wateja wetu, tunawapima vizuri, na tunawapa matibabu na wale wanashida inayohitaji dawa tunawapa dawa Bure kabisa hivyo mwitikio ni mzuri na wagonjwa ambao wamekuja bila taarifa Maalum ( appointment ) wengi tu nao tunawasaidia.

Mmoja wa wakazi wa Mwanza Emilia Siara amesema alipata kusikia matangazo kwamba wanatoa huduma ya kucheki afya ya  Moyo, alikwenda na kuhudumia vizuri sana, na huku wakifanya ufuatiliaji wa wa Hali inayoendelea ya mgonjwa, nikapewa matokeo yangu na Niko sawa.

" Nilichofurahia ni madaktari wanavyofuatilia hali ya mgonjwa, kitu hiki tumekiona leo tu ndivyo ilivyo au kunakua na mabadiliko, kwahiyo leo wakanishauri kuja tena kwaajili ya kufanya mwendelezo wa kuchunguza zaidi ( Check up ) kwa hiyo nimechunguzwa kwa mara ya pili na kesho pia natakiwa kuja Kwa ajili ya mfuatiliao wa uchunguzi ( checkup ).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...