Na Nasra Ismail, Geita

Takribani shilingi mil 18 zitatumika katika mradi wa kupeleka umeme katika maeneo ambayo yanajihusisha na shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa  madini unaojulikana kwa jina la (SMALL MINING).

Akitoa taarifa hiyo wakati wa semina ya wadau wa nishati meneja wa TANESCO Grace Ntungi alisema kuwa mradi huu utatekelezwa kanda yote ya ziwa huku ikihusisha  mikoa za Mwanza,Geita Simiyu,Mara  na kagera.

Mradi huu ambao unafadhiliwa na REA wakala wa nishati ya umeme vijijni umeshaanza kutekelezwa na una mkataba wa miezi 18 tu.Aidha bi grace aliutaja mradi mwingine kuwa ni mradi wa kupeleka umeme katika migodi ya madini ya GGML ambapo hapo awali walitumia jenereta ili kuzalisha nishati za umeme.

Mradi huu ambao umefadhiliwa na TANESCO ambao utagharimu kiasi cha sh bil 7 hivyo utasaidia kupunguza gharama kubwa ya uendeshaji.

Grace aliongeza kuwa hali ya upatikanaji wa umeme ni nzuri ingawa si kwa asilimia mia moja kutokana na changamoto mbalimbali ambayo zinalikumba shirika hilo.

“lengo letu kuu ni kuhakikisha kwamba umeme unapatikana kila wakati na tatizo la upande mmoja lisisababishe tatizo upande mwingine”Alisema Grace

Aliitaja miradi tarajiwa kuwa ni mradi wa kupoza Bukombe,  pamoja na ujenzi wa kituo kidogo cha kusambaza umeme Buchosa Sengerema ili kwafikia wachimbaji wadogo pia.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...