Na Janeth Raphael - Michuzi Tv Dodoma


Wadau wa Kilimo Hai wamekutana jijini Dodoma kwa siku moja kuuthibitisha Mkakati wa Kitaifa wa Kilimo Ikolojia Hai, mkakati utakaotoa taswira ya mwelekeo wa utekelezaji Kilimo Hai hapa nchini.

Kikao hicho cha uthibitishahi kimefunguliwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango(DPP) wa Wizara ya Kilimo, Obadiah Nyagiro ambapo amebainisha kuwa kati ya mambo yaliyopo kwenye mkakati huo ni pamoja na kutoa mwongozo kwenye suala la zima la upatikanaji wa Pembejeo, Mbegu na Matumizi ya
teknolojia.

Pia amebainisha kuwa mkakati huo utatoa taswira nzima ya uwepo wa Masoko, Utaalamu wa Kilimo hao kwa watendaji pamoja na masuala mengine mtambuka yatakayochagiza ufanisi wa Kilimo Hai nchini.

Amewataka washiriki wa kikao kuhakikisha kuwa mkakati huo unaeleweka vema kwa wananchi.

Amesema mkakati huo unapaswa utoe kipaumbele kwenye utafiti utakaosaidia upatikanaji wa mbegu bora zenye tija kwa kilimo hai.

" Nawasisitizia kuwa mkakati huu unaothibitisha leo katika maoni yenu hakikisheni kuwa mnazingatia maslahi ya taifa kwa kukiwezesha kilimo kilete tija hasa kwa kuhakikisha kunakuwa na mbegu bora na zisiwe zenye kemikali yani mkakati utofautishe mazao ya kilimo ikolojia hai na yale ya kemikali" amesema Nyagiro

Kikao hicho pia kimeshirikisha wadau wa kilimo hai kutoka kila kona ya nchi ambapo wamepata fursa ya kutoa maoni yao kuhusiana na nini kiongezwe kwenye mkakato huo.

Ayesiga Buberwa ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Islands of Peace Tanzania amesema kuwa hiyo ni hatua kubwa na ya kujivunia kwa wadau wa kilimo hai kuwa na mkakati.

"Kikao cha leo cha tathmini ya mkakati wa kuendeleza kilimo hai ni hatua kubwa na muhimu katika kuimarisha kilimo hai hapa nchini, kama wadau tunatmia wasaha huu kutoa maoni yetu na kuhakikisha yanaingizwa kwenye mkakati yakawe mwanga wa kilimo hai nchini" amesema Ayesiga.

Kikao hicho kilichoandaliwa na Wizara ya Kilimo chini ya uratibu wa TOAM ambapo Mkurugenzi wake Bakari Mongo amesema kuwa ana imani kuwa mkakati huo unaoenda kuanza kazi hivi karibu utachangia kukuza kilimo hai na kuwa mazao yatokanayo na Kilimo Hai yanaenda kuchangia vilivyo pato la taifa.

Anasema kuwa yapo mazao mengi yatokanayo na kilimo hai yanatakiwa nje ya nchi ambapo ameyataja mazao kama parachichi, pilipili, kahawa pamoja na viungo hasa kutoka Zanzibar na yanatakiwa zaidi nchi za Ujerumani, Denmark na kuwataka vijana kuchangamkia fursa.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Kilimo, Obadiah Nyagiro akisisitiza jambo wakati wa warsha ya kuthibitisha Mkakati wa Kitaifa wa Kilimo Ikolojia Hai kilichofanyijka jana Mjini Dodoma. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...