Na Fauzia Mussa, Maelezo

 

Wadau wa Maziwa wametakiwa kuchukua  tahadhari wakati wanapozalisha na kusambaza bidhaa hiyo  ili kuimarisha na kulinda Afya ya Mtumiaji.

 

Akiwasilisha mada ya udhibiti wa Usalama wa Bidhaa za Maziwa wakati wa mafunzo ya usalama wa chakula kwa Wafugaji,Wauzaji na Wasarifu wa Maziwa  Ofisa Kutoka ZFDA Thamra Khamis Talib amesema maziwa hupitia hatua nyingi kabla ya kufika kwa mtumiaji ikiwemo ukamuaji na utunzaji hivyo mashirikiano ya pamoja yanahitajika ili kuhakikisha yanamfikia mtumiaji katika hali ya usalama.

 

Alisema maziwa yanaweza kuchafuka wakati yanapoingizwa  katika vyombo visivyosafishwa vizuri ikiwemo chupa za plastiki na Vidumu hivyo aliwataka wadau hao kuacha kutumia vifaa hivyo kwani vinakua na vimelea vingi ambavyo haviwezi kuondoka kwa kukoshwa kwa  maji na sabuni.

 

Aliongeza kuwa  vifaa hivyo sio salama kwa afya ya mtumiaji  na kuwataka wadau hao kuhifadhi maziwa katika chupa za vigae au vyombo vinavyoweza kuingia mkono wakati wa kusafisha.

 

Alifahamisha kuwa baadhi ya wauzaji hupokea maziwa safi kutoka kwa Mfugaji na kukaguliwa na ZFDA  lakini mara  baada ya ukaguzi huchafua maziwa hayo kwa maslahi binafsi  na kuhatarisha afya za jamii.

 

“Ukaguzi wa ZFDA unafanyika wakiondoka tu wauzaji wanafanya ghushi watajaza maji waweke na samli ili yaonekane maziwa safi yenye mafuta  kwa lengo la kupata faida zaidi kwa hali hii tutafika”alihoji Mwasilishaji

 

Alisema kuwa  kuna  baadhi ya Wauzaji huingiza vitu visivyohitajika katika maziwa kama samli , au siagi  hali inayopelekea kuchafuka kwa bidhaa hiyo,  hivyo aliwataka watumiaji kuacha kununua maziwa kama hayo kwani  uchafuzi mwengine ni wawazi wala hauhitaji utaalamu na vipimo vya maabara.

 

“utayakuta maziwa juu yana rangi ya njano kabisa ya siagi unamimina chini kuna unga unga bado unaendelea tu kutumia maziwa hayo,tunavyoendelea kununua bidhaa hii kwa wauzaji kama hawa ndio tunawapa nguvu ya kuendelea kuharibu  afya zetu”alisistiza Mwasilishaji huyo

 

Akifungua mafunzo ya kuwajengea uelewa Wadau hao juu ya usalama wa Chakula Mratibu  wa mradi wa kudhibiti Sumu kuvu ZFDA  Aisha Sleiman amesema  wadau wengi wa maziwa hawana elimu hiyo, hivyo mafunzo  hayo yatawasaidia kujua njia sahihi ya kuhifadhi maziwa na kuhakikisha hayachafuki na kubaki  salama hadi kufika kwa mtumiaji.

 

Alisema Serikali  imeimarisha Idara ya udhibiti na maabara ya Dawa na Chakula  Zanzibar kwa lengo la kumlinda mtumiaji , hivyo ZFDA itaendelea kukagua vyakula vyote ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha usama wa chakula kabla ya kuuzwa kwenye masoko ya ndani na nje ya Nchi.

 

Hata hivyo aliitaka jamii kushirikiana kwa pamoja kuweza kulinda na kuimarisha Afya ya mtumiaji  kwa kutoa taarifa za uwepo wa chakula kisicho salama katika jamii

 

Washiriki wa mafunzo hayo Asia Mwinyi Bai, Suleiman Bakar simba na Salum Rehani  Wameiomba Serikali  kuwawakea viwanda vyenye mitambo ya kuchakatia maziwa  na vifungashio vyenye ubora ili kuweza kuingiza bihaa zao katika hoteli za kitalii, nakuuzika nje ya Nchi.

 

Hata hivyo Washiriki hao wameiomba ZFDA kuandaa mafunzo kama hayo kwa mtumiaji ili kuongeza nguvu ya ulinzi wa  afya za Jamii.

 

Awali walishukuru kwa kuwapatiwa  mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi  ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

 

 Mafunzo hayo ya siku moja yaliwashirikisha wadau wa maziwa kutoka Vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali Mjini na Vijijini.

Wadau wa Maziwa wakifuatilia mafunzo ya  kuwajengea uelewa juu ya udhibiti wa bidhaa za chakula na mifugo huko Ofisi za Wakala wa dawa na chakula Mombasa Zanzibar .
Mkaguzi wa  chakula ZFDA  Mwajuma Ali akiwasilisha mada ya usalama wa chakula wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa Wadau wa Maziwa juu ya udhibiti wa bidhaa za chakula na mifugo huko Ofisi za Wakala wa dawa na chakula Mombasa Zanzibar

Mratibu  wa mradi wa kudhibiti Sumu kuvu ZFDA  Aisha Sleiman akiwasilisha mada ya udhibiti wa sumu kuvu katika bidhaa za mifugo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa wadau wa Maziwa juu ya udhibiti wa bidhaa za chakula na mifugo huko Ofisi za Wakala wa dawa na chakula Mombasa Zanzibar 

 

PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...