Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro , akizungumza na Waislam wa Kata ya Mtinko wakati wa harambee ya ujenzi wa msikiti iliyofanyika Septemba 3, 2023.

................................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

WADAU mbalimbali wameombwa kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Jaamigh uliopo Kata ya Mtinko Wilaya ya Singida, mkoani Singida ambapo jumla ya Sh. Bilioni 1.8 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo.

Katibu wa kamati ya ujenzi wa msikiti huo, Abdallah Rajab akizungumza wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa msikiti huo mbele ya Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro alisema hadi kukamilika kwa ujenzi huo Sh.Bilioni 1.8 zinahitajika.

Rajab alisema msikiti wa awali ambao ulijulikana kama Msikiti wa Ijumaa Mtinko ulijengwa mwaka 1949 ukiwa na uwezo wa kuhudumia waumini 100 kwa wakati mmoja.

Alisema kutokana na ongezeko la waumini msikiti huo ulipanuliwa mwaka 1990 na kuwa na uwezo wa kuwahudumia waumini 300 na unatumika hadi hivi leo.

Rajab alisema kutokana na ongezeko la waumini na kuanza kuswalia nje mwaka 2018 ndipo walipopata wazo la kuanzisha ujenzi wa msikiti wa sasa wa ghorofa ambao ujenzi wake ulianza mwaka 2019.

'' Ujenzi upo hatua ya kusuka bimu kwenye msingi na ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia waumini 1000 kwa wakati mmoja,'' alisema Rajab.

Alisema msikiti huo utakuwa na huduma za ofisi ya utawala, madrasa, vibanda vya biashara na huduma ya vyoo.

Alisema mahitaji makubwa ya hivi sasa ya ujenzi huo ni mchanga, saruji na nondo na kuwa katika hatua hiyo waliyoifikia ya ujenzi zimetumika Sh.Milioni 28,059,300 fedha zilizotokana na sadaka za waumini na wadau wengine mbalimbali na kuwa kwenye akaunti yao wana Sh.Milioni 3.

Baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa msikiti wakishirikiana na kamati ya bodi ya msikiti, Jumuiya ya Wanawake wa Wakiislam } JUWAKITA }, wa kata hiyo na kamati ya ujenzi ilifanyika harambee ambapo zilipatikana zaidi ya Sh.Milioni 3.7.

Katika kuongeza nguvu ya kupatikana kwa fedha za ujenzi wa msikiti huo Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro anatarajia kufanya harambee nyingine hivi karibuni katika tarehe itakayo pangwa ambayo itawashirikisha wadau na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Mkoa wa Singida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...