WANAHARAKATI wamepewa ujuzi wa kukabiliana na changamoto ya afya ya akili wakiwa katika mazingira ya kazi au nyumbani ili kuhakikisha kupungua kwa matatizo hayo kwenye jamii ambapo inaonekana tatizo hilo limekithiri.

Akizungumza leo Septemba 13,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwezeshaji wa Semina hiyo Bi.Sylivia Sosthenes amesema kupitia semina hiyo itasaidia kuangalia wanaharakati na Afya zao za akili na yale wanayo kumbana nayo katika harakati, kuanzia familia zao,wanakutana na kesi ngapi na lipi suluhisho la Afya zao za Akili.

"Matokeo ya Semina hii ni kuepuka matukio ambayo ni ya kikatili yasipelekee Changamoto ya Afya ya akili ".

Aidha Bi Sylivia Amesema sababu zinazo pelekea matatizo ya Afya ya akili,ni pamoja na ukatili wa kijinsia, Changamoto za kiuchumi,maswala ya malezi, mahusiano kazini au nyumbani.

Pamoja na hayo amesema dalili za Changamoto ya Afya ya akili Ni pamoja na mtu kujitenga,mtu kutokujijali au kuleta viashiria vya kujitoa uhai au kumtoa mtu uhai.

"Mtu mwenye tatizo la Afya ya akili kwa mtu ambaye si mtaalamu anatakiwa amuoneshe sehemu ya kwenda au kumpatia ushauri wa awali,na kwa mtu ambaye Ni mtaalamu anatukiwa kumshauri na kumfanyia rufaa kwa wataalamu wengine,maana Changamoto hii ina athiri wakati mwingine Hadi mwili." amesema





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...