Na.Khadija Seif,Michuziblog

VIJANA 24 wanatarajiwa kunufaika na onesho maalum la bingwa kwa kupewa mitaji kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kimaendeleo na kutimiza ndoto zao.

Akizungumza na Wanahabari Jana 17,2023 katika ofisi za Tv3 Jijini Dar es Salaam Msimamizi wa vipindi wa Tv3 Emanuel Sikawe kwenye uzinduzi wa msimu wa pili wa onesho hilo chini ya udhamini wa Startimes Media.

Sikawe, onesho hilo lililoanza rasmi mwaka jana, linawapa nafasi vijana kuonesha uhalisia wa maisha yao ya kila siku katika jumba maalum ambapo wakiwa huko hupewa mafunzo ya ujasiriamali, matumizi mabaya ya dawa za kulevya na mitandao ya kijamii.

“Lengo lake ni kuwawezesha vijana kufahamika na kufikia malengo ya ndoto zao katika maisha. Kipindi hiki cha Tv kimesaidia vijana wengi sana hapa nchi katika masuala ya elimu ya afya ya akili, kujitegemea na kutatua changamoto mbalimbali katika maisha yao ya kila siku."

Amesema vijana hao waliochaguliwa kutokana na ushawishi wao kwenye mitandao ya kijamii hukaa ndani ya jumba hilo kwa wiki 11 ambapo watakuwa wanaonekana kupitia Tv3 katika vipindi 65 vitakavyorushwa kuanzia Jumapili mpaka ijumaa.

Meneja Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa amesema msimu huu wa onesho hilo utakuwa tofauti kwani wameandaa zawadi kubwa zaidi ya msimu wa kwanza.

“Kazi yetu kubwa Startimes ni kuleta Maudhui, msimu huu utakuwa wa kutofautisha hata zawadi itakuwa kubwa zaidi ya msimu uliopita, tutaitaja baadaye."

Malisa amegawa zawadi za ving’amuzi kwa washiriki hao kwa ajili ya kugawa kwa familia zao ili waweze kuwafuatilia na kupata nafasi ya kuwapigia kura.

Mwisho wa onesho hilo baada ya wiki 11 atapatikana mshindi mmoja ambaye ataondoka na fedha na zawadi nyingine mbalimbali huku waandaaji hao wakiomba wadhamini wengine wajitokeze kuunga mkono vijana hao kuwasaidia kutimiza ndoto zao.
Msimamizi wa vipindi kutoka Tv3 Emmanuel Sikawa akizungumza na Wanahabari na washiriki 24 wa Shindano la Bingwa na kueleza mchakato wa jinsi Shindano lilovyoanza na namna linakwenda kubadilisha maisha ya watu na washiriki hao wengi wenye ushawishi mitandaoni hivyo jamii itanufaika namna ya kutumia mitandao ya kijamii katika kujiongezea kipato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...